Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Siasa na Mahusiano ya Kimataifa wa CCM, Rabia Hamid, amefanya ziara leo 2 Julai katika Mikoa ya Manyara na Kilimanjaro. 

Akiwa mkoani Manyara, Rabia alipokelewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara, Ndugu Petter Toima, kabla ya kushiriki kikao cha Kamati ya Siasa na Halmashauri kuu ya Mkoa, ambapo aliwataka wajumbe kuendelea kuimarisha umoja na ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya chama pamoja na kusimamia kwa ufanisi miradi ya CCM.

“Wajumbe wa Kamati ya Siasa tuwe na umoja na ushirikiano katika kuimarisha chama na kusimamia miradi pamoja na kutekeleza maelekezo ya chama. Tuache siasa za makundi,” alisema Rabia.

Baada ya kumaliza ziara yake mkoani Manyara, Rabia aliendelea na ziara ya ulezi mkoani Kilimanjaro ambako alishiriki kikao cha Kamati ya Siasa ya Mkoa na kupokelewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi.

“ Umoja na amani ni msingi wa mafanikio ya chama chetu. wajumbe tuendelee kudumisha umoja, mshikamano na amani tushirikiane, tuheshimiane na tuendelee kutekeleza majukumu yetu kwa maslahi ya chama na Taifa,” alisema katika kikao cha Kamati ya siasa na Halmashauri kuu ya Mkoa Kilimanjaro.

Ziara ya Rabia katika mikoa ya Manyara na Kilimanjaro ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya ulezi yenye lengo la kuimarisha uhai wa chama, kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya chama na kusikiliza maendeleo ya shughuli mbalimbali katika mikoa hiyo.
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...