Na Janeth Raphael MichuziTv
Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zimeandika historia baada ya kufanikisha kwa mara ya kwanza upasuaji wa kuziba matundu ya moyo kwa watoto kutoka nchini Burundi, hatua inayotajwa kuwa mafanikio makubwa katika kuimarisha huduma za kibingwa na kukuza tiba utalii nchini Tanzania.
Mafanikio hayo yametangazwa na Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Prof. Abel Makubi, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema ushirikiano kati ya BMH na JKCI unaendelea kuzaa matokeo chanya na utaimarishwa zaidi ili kuongeza wigo wa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kwa Watanzania pamoja na wagonjwa kutoka mataifa jirani.
Prof. Makubi amesema hatua hiyo ni ya kihistoria kwa kuwa ndiyo mara ya kwanza kwa taasisi hizo mbili kushirikiana kuwafanyia watoto kutoka nje ya Tanzania upasuaji wa moyo, jambo linaloonesha uwezo wa nchi katika kutoa huduma za matibabu zinazokidhi viwango vya kimataifa.
Amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha wagonjwa kutoka ndani na nje ya mipaka yake wanapata huduma bora za kibingwa bila kulazimika kusafiri kwenda mataifa ya mbali kutafuta matibabu yanayopatikana hapa nchini.
"Kwa miaka mingi tumekuwa tukishuhudia wagonjwa wakisafiri kwenda nje kwa huduma ambazo sasa zinaweza kutolewa nchini kwa ufanisi na kwa gharama nafuu zaidi. Dhamira yetu ni kuona Tanzania inakuwa kitovu cha huduma za matibabu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kwingineko," amesema Prof. Makubi.
Akizungumzia hali za wagonjwa hao, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Kifua, Dk. Ahmed Toure, amesema watoto waliopatiwa matibabu walizaliwa na matatizo ya kimaumbile ya moyo yaliyokuwa yakihitaji upasuaji maalumu ili kurekebisha mfumo wa mzunguko wa damu.
Amefafanua kuwa baadhi ya watoto wenye matatizo hayo huzaliwa na hitilafu kwenye mishipa ya moyo inayosababisha damu kutosambaa ipasavyo kwenda kwenye mapafu na sehemu nyingine za mwili, hali ambayo inaweza kusababisha madhara makubwa endapo matibabu hayatatolewa mapema.
Kwa mujibu wa Dk. Toure, watoto wengi huanza kuonesha athari kubwa wanapofikisha umri wa miezi sita hadi mwaka mmoja, hivyo uchunguzi wa mapema na upasuaji kwa wakati ni muhimu katika kuongeza nafasi ya kuishi maisha marefu na yenye afya.
Naye Mratibu wa Tiba Utalii Tanzania, Dk. Asha Mahita, amesema mafanikio hayo yanaendana na malengo ya Serikali kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ambayo inalenga kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha huduma za tiba utalii katika ukanda wa Afrika.
Amesema kuwapokea na kuwatibu wagonjwa kutoka Burundi ni ushahidi kuwa uwezo wa wataalamu wa afya nchini unaendelea kuimarika na kwamba huduma zinazotolewa sasa zinavutia wagonjwa kutoka mataifa mengine.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha wagonjwa wanaendelea kufuatiliwa baada ya upasuaji ili kuhakikisha wanapata nafuu kamili na kuendelea kuishi maisha yenye afya.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa Mbobezi wa Upasuaji wa Moyo kwa Watoto kutoka JKCI, Dk. Godwin Godfrey, amesema ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili umeongeza uwezo wa wataalamu kubadilishana uzoefu na kuendelea kuboresha huduma za kibingwa nchini.
Ameeleza kuwa ushirikiano huo unachangia kuwafikia wagonjwa wengi zaidi, kuongeza ujuzi kwa wataalamu wa afya na kuwezesha hata wananchi wasio na uwezo mkubwa wa kifedha kupata huduma za matibabu zenye ubora wa hali ya juu.
Kutoka Burundi, Dkt. Nzitunga Aimee Jean Carmen Octavie wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Gitega ameishukuru Serikali ya Tanzania pamoja na uongozi wa BMH kwa kuwakaribisha na kuwapatia watoto wao matibabu salama.
Amesema mafanikio hayo yanaimarisha zaidi uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Burundi, huku yakitoa matumaini mapya kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za kibingwa katika ukanda huo.
Naye mzazi wa mmoja wa watoto waliopatiwa upasuaji, Shedrack Nzigiyimana, amesema ameridhishwa na huduma alizopata mtoto wake na kushukuru wataalamu wa afya pamoja na Serikali ya Tanzania kwa kuwapa fursa ya kupata matibabu yaliyobadili maisha ya mtoto wake.
Amesema ukarimu na ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi umewezesha watoto wao kupata huduma muhimu ambazo zingekuwa vigumu kuzipata kwa wakati, huku akieleza matumaini kuwa ushirikiano huo utaendelea kuwasaidia wagonjwa wengi zaidi kutoka nchi zote mbili.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...