NA MWANDISHI WETU



DIWANI wa Kata ya Kinondoni, wilayani Kinondoni, mkoani Dar es Salaam, Idrissa Said Ngatiche (CCM), amesema atafanya jitihada kubwa kuhakikisha watu wenye ulemavu katika kata hiyo wananufaika na kuzifikia fursa muhimu hususan ni za kiuchumi.

Ameyasema hayo leo katika mkutano wa Siku ya Watu Wenye Ulemavu Kinondoni, aliyoandaa maalumu kusikiliza na kutatatua kero za kundi hilo, kula chakulacha pamoja na kukabidhi msaada wa viti mwendo viwili.

Ngatiche amesema, kundi hilo ni muhimu kushirikishwa kikamilifu katika shughuli za kiuchumi ikiwemo kunufaika na mikopo ya asilimia 15 inayotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa vikundi vya wajasiriamali wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

"Kutokana na hali hiyo leo nimeandaa Siku Maalumu ya Watu Wenye Ulemavu Kinondoni, kwa nia ya kuwatambua, kujua idadi yao na kuwasikiliza changamoto zao.Kundi hili limekuwa likisahaulika sana, hivyo kama diwani nimetumia jukwaa hili leo kuwakusanya pamoja ili wanufaike na fursa zilizopo kama makundi mengine,"amesema Ngatiche.

Ameeleza huo ni mwanzo wa hatua zake za kulisaidia kundi hilo huku akitoa wito kwa jamii kuto kuwaficha watu wenye ulemavu hususan watoto ambao wanatakiwa kwenda shule.

"Jamii isiwafiche watu wenye ulemavu. Serikali yetu chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, haijawatenga ndiyo maana katika ile mikopo ya asilimia 15 inayotolewa na halmashauri inatenga asilimia mbili kwaajili ya vikundi vya wenye ulemavu,"ameeleza Ngatiche.

Diwani huyo, amekabidhi viti mwendo viwili kwa watu wenye ulemavu wawili ambao ni mtoto Brighton Michael na mtu mzima Daud Anthon.

Mwenyekiti wa Watu wenye Ulemavu hao Ali Maulid Ali, amempongeza Diwani Ngatiche, kwa jitihada zake za kuwatambua na kuwasaidia watu wenye ulemavu kwani kundi hilo limekuwa likisahaulika.

Maulid amesema kundi kundi hilo linanguvu na halipo kinyonge na mutano huo ni chachu ya kuanzisha umoja wenye nguvu wa watu wenye ulemavu.

" Tunamshukuru sana Rais dk. Samia, nchi iko salama. Yakitokea machafuko sisi wenye ulemavu ndiyo waathirika wakubwa, hivyo tuwakemee watu wanao chochea machafuko. Mkutano huu uwe mwanzo wa sisi watu wenye ulemavu kuwa na umoja wenye nguvu. Hivyo tunamshukuru pia Diwani Ngatiche kwa kuliona hili,"alieleza Maulid.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...