Halmashauri ya Wilaya ya Geita imetoa mifuko 50 ya saruji kuwezesha ujenzi wa ghala la kisasa la kuhifadhi mazao Kata ya Bukoli.

Msaada huo umetolewa Julai 11, 2026 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Karia Rajab Magaro wakati wa harambee iliyoongozwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu  TAMISEMI Dkt. Jafar Rajab Seif ukumbi wa Gwila.

Akizungumza katika harambee hiyo, Magaro amesema Halmashauri itaendelea kutoa ushauri wa kitaalamu kupitia wahandisi na maafisa kilimo ili ujenzi wa ghala hilo ufanyike kwa viwango. 

"Tutahakikisha kikundi kinasajiliwa kwa wakati. Tunawasihi msishirikishe wahandisi wa Halmashauri katika kila hatua ili mradi huu uwe na tija kwa wakulima," amesema Magaro.

Kwa upande wake Dkt. Seif ameipongeza Halmashauri ya Geita kwa kuweka mazingira wezeshi kwa vikundi vya wananchi. Amesisitiza umuhimu wa vikundi hivyo kuwa mfano wa kuigwa na vingine nchini.

"Serikali itaendelea kuwezesha vikundi kupitia mikopo iliyoidhinishwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuongeza ajira na kuimarisha uchumi wa wananchi," amesema Dkt. Seif.

Mwenyekiti wa Kikundi cha Amani Group Bukoli Issa Masanzu ameishukuru Serikali kwa sera na mipango inayowawezesha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Ghala hilo la kisasa lenye ukubwa wa mita 48 kwa 38 linatarajiwa kugharimu shilingi milioni 200. Mradi huo unalenga kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao, kupunguza upotevu baada ya mavuno na kuongeza kipato cha wakulima wa Bukoli na maeneo jirani.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...