Kituo cha Uzalishaji na Ukuzaji wa Viumbe Maji cha Lubambangwe kilichopo Chato Mkoa wa Geita, kimefikia asilimia 80 ya utekelezaji. Kituo hicho kiko chini ya Wizara ya Uvuvi na kinatarajiwa kuhudumia wafugaji wa samaki kutoka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.

Hayo yamebainishwa na Kamati ya Siasa na Utekelezaji ya CCM Mkoa wa Geita wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo wilayani hapa.

Akitoa taarifa, Kaimu Ofisa Mfawidhi wa Kituo hicho Bilali Banali amesema kituo hicho kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya samaki laki tatu kwa mwezi pamoja na kuzalisha vyakula vya samaki.

Amesema lengo la kituo hicho ni pia kukusanya zaidi ya shilingi milioni 180 kwa mwaka kupitia utoaji wa vibali vya viranga na vizimba kwa wafugaji.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita Waridi Mngumi amewataka wananchi kulinda kituo hicho ili kiweze kuwanufaisha kiuchumi.

Amesema kituo hicho kimejengwa kwa kuzingatia Falsafa ya Uchumi wa Buluu kwani kitatoa pia mafunzo mafupi kwa wananchi kuhusu ufugaji wa samaki na uzalishaji wake.

















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...