
KAMANDAwa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro ameridhishwa na ushirikishwaji wa vijana katika uendelezaji wa miradi ya gesi asilia inayoendelea mkoani Mtwara.
Akizungumza katika banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kwenye maonesho ya Sabasaba Kamanda Muliro amesema ni vema miradi hiyo ikaendelea kushirikisha vijana kwani serikali inaendelea kutoa hamasa kwa vijana kujikita katika sekta ndogo ya mafuta na gesi.
Kwa upande wake Mjiolojia kutoka PURA Lukelo Matimbwi amemueleza Kamanda Muliro kuwa katika mradi wa uzalishaji wa gesi asilia unaoendelea Mnazi Bay zaidi ya asilimia 90 wanaofanya kazi hapo ni vijana wa kitanzania.
Ameongeza kuwa katika mradi wa uzalishaji wa gesi asilia Songo Songo pia ushirikishwaji wa vijana wa kitanzania ni mkubwa sana katika utekelezaji wa mradi huo.
Kamanda Muliro ametembelea banda la PURA kwenye Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...