Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi baada ya tafiti, kubadilishana uzoefu na stadi mbalimbali kutoka kwa Nchi zenye mbinu bora,teknolojia ya juu pamoja na uzoefu mkubwa wa kukabiliana na uhalifu,Amezindua Programu Maalumu ya Usalama,Maendeleo na Samia ambayo pia itashirikisha hatua za Mafunzo na Vifaa vya Kisasa kutoka nchi zilizoendelea Kiusalama lengo ikiwa ni kuimarisha na kuhusianisha Usalama na masuala ya Amani na Maendeleo Tanzania bara na visiwani .
Waziri Katambi amezindua Programu hiyo leo,jijini Dar es Salam katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo akizungumza na mamia ya wafanyabiashara,machinga,madereva bodaboda,mamalishe na babalishe amesema suala la amani na usalama ni jukumu la kikatiba la serikali iliyochaguliwa na wananchi.
Amesisitiza kuwa kipaumbele cha Rais Samia ni Nchi Kwanza, Wananchi kwanza na Uchumi kwanza.
“Wizara hii ina dhamana ya masuala ya Ulinzi na Usalama, ina dhamana ya ulinzi wa kila raia, ina dhamana ya ulinzi wa kila mali ya raia, ina dhamana ya ulinzi wa Rasilimali za Taifa pamoja na mali za Taifa zinazomilikiwa na Umma" alisema Katambi
“Taarifa yoyote,maelezo yoyote,kauli yoyote,uchochezi wa aina yoyote unaolenga kuhatarisha amani ya mtu mmoja ambae ni raia wa Tanzania,sisi kama Serikali kwa mujibu wa katiba ya mwaka 1977 Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali zao na rasilimali za nchi ni jukumu la Serikali kwa kuhakikisha wananchi wanakua salama kwenye mazingira ya uzalishaji na shughuli za maendeleo”aliongeza Waziri Katambi
Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa wafanyabiashara,bodaboda,machinga,babalishe na mamalishe walisema wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwawekea mazingira sahihi ya kufanya shughuli zao huku wakiweka wazi nia yao ya kutotumika na kikundi cha watu wachache wanaotaka kuchafua amani ya nchi.
Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Ayoub Mohammed Mahmoud,Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo,Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,SACP William Mkonda,Viongozi wa Wafanyabiashara,Bodaboda,Wamachinga,Mamalishe na Babalishe pamoja na wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...