KUNA wakati kama binafamu wenye akili timamu lazima tutafakari mambo yanayoendelea nchini na kwa siku ya leo tujadili kidogo kuhusu michango ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).


Ndio lazima tujadili maana imekuwa gumzo kila kila kona, sio kwasababu michango inadaiwa kutafunwa na baadhi ya viongozi wa Chama hicho, hapana.Nazungumzia kuhusu kusuasusa kwa michango yenyewe.

Ni kama wachangiaji wameshutuka kwamba fedha wanazotoa zinaliwa na wajanja wachache lakini kubwa zaidi waliokuwa wanakichangia kwa muda mrefu wakiwemo wafanyabishara wameona chama hicho kimepoteza muelekeo,hakina mvuto.

Ile Kampeni ya Tonetone ya kuchangia CHADEMA imedoda kabisa .Na hivi karibuni tumesikia tuhuma za michango kutafunwa na wachache.

Hata hivyo katika hili la michango ya CHADEMA kuonekana inasuasua ni vema kwanza tukarudi mwanzo kule wakati Chama hicho kimeanza mwaka 1992 baada ya kuanza kwa Mfumo wa Vyama vingi nchini Tanzania.

Wakati chama hicho kinaanza waanzilishi wake walikuwa mchanganyiko wa wanasiasa, wanaharakati, watu maarufu na wa sekta binafsi waliotaka mfumo wa kisiasa unaoweka msisitizo katika uwajibikaji na uhuru wa kiuchumi.

Miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa wakatiCHADEMA inaanza walikuwepo akina Edwin Mtei(sasa marehemu)Mwanasheria mashuhuri Bob Makani na wengine wengi.Hata Ndesamburo naye ni miongoni mwao.

Ukweli watu hao wa mwanzo kabisa hawakuwa wanamapinduzi, bali walikuwa wanakapitalisti waliochoshwa na uendeshaji wa Serikali ya wakati huo.

Kutokana na mipango na mikakati ya CHADEMA kwa wakati ule ilishuhudiwa wafadhili wa awali wengi wao wakiwa ni wafanyabiashara na sekta binafsi.

Katika miaka ya mwanzo, CHADEMA ilivutia msaada wa watu wenye uwezo na wafanyabiashara waliotaka sera zinazorahisisha biashara na uwekezaji.

Michango hiyo mara nyingi haikuonekana hadharani; ilitolewa kwa njia za ndani au kwa msaada wa kimkakati ili kuimarisha miundombinu ya chama na kampeni za kukujenga chama mikoani. Kujiunga kwa viongozi wenye umaarufu kuliongeza mvuto wa chama kwa wafadhili na wafuasi.

Pia ilikuwa ni jambo la kawaida kusikia Mfanyabiashara maarufu Mustafa Jafari Sabodo (sasa marehemu) akitoa mamilioni ya fedha kwa Chama hicho na ndoto yake ilikuwa ni kuona Chama hicho kinakuwa na Ofisi yake.

Ndoto ya Sabodo haikutimia maana licha ya kutoa zaidi ya milioni 100 hazikutumika kujenga ofisi.Sijui zilitumika wapi? Zile fedha hazikujulikana zilikwenda wapi.CHADEMA bwana wajanja wajanja sana.

Ukweli katika miaka 1995 mpaka miaka ya 2010 CHADEMA ilikua kwa kasi kubwa na mwaka 2014 baada ya Edward Lowassa alipotangaza kujiunga na Chama hicho kikakua zaidi.Tukashuhudia gumzo kubwa kwa chama hicho na umaarufu mkubwa katika historia ya siasa za vyama vingi nchini Tanzania.

Kujiunga kwake Lowasa kulionyesha uwezo wa CHADEMA kuvutia viongozi wa ngazi ya juu kutoka upande wa pili wa kisiasa. Mabepari walifungua mikoba yao, wakimimina fedha nyingi kuunga mkono chama.

Hata hivyo, kila kitu kilibadilika baada ya kuingia kwa uongozi mpya wa Tundu Lissu. Uongozi wake na wa viongozi wenzake wa kisiasa uliashiria mabadiliko ya mkazo wa chama kuelekea masuala ya haki za kiraia, uwazi, na masuala ya kijamii.

Hiyo ilileta mabadiliko ya mtazamo wa chama ambayo baadhi ya wafadhili waliona hayakuwa ya kuendeleza maslahi ya kiuchumi.

Pamoja nayo hayo tangu CHADEMA ilipofanya mabadiliko ya uongozi wake wa ngazi za kuu tunashuhudia athari na changamoto za mabadiliko hayo.

Mabadiliko hayo ya mwelekeo wa chama yameathiri pia chanzo cha ufadhili kwa operesheni za CHADEMA kwenye nyanja kadhaa. Ni wazi CHADEMA imepoteza uaminifu wa wafadhili wa sekta binafsi.

Haswa kundi la wafanyabiashara wanaotaka sera za soko huria wamesita kuendelea kutoa michango baada ya chama kuoonyesha msimamo wakisoshalisti au kinachokosoa tu sekta binafsi bila kujaribukuelewa changamoto zao.

Upungufu wa rasilimali za kampeni umeonekana wazi, bila michango kubwa, chama kinakosa uwezo wa kuendesha kampeni za kitaifa, kulipa miundombinu ya chama, na kumudu gharama za kisheria na mahitaji ya wanachama.

Hizo ni baadhi ya atahari za madiliko yaliyotokana na chama kilijikita na wanaharakati ambao wanaamini"wafanyabiashara hawana shida." Mabadiliko ya mwelekeo bila mkakati wa kuunganisha tabaka tofauti za wafuasi(wafanyabiashara, wanaharakati, wanasiasa wa jadi) umeacaha pengo la utekelezaji.

CHADEMA sasa inahitaji sera zinazoonyesha jinsi masuala ya kijamii (kama kupunguza umaskini) yanavyoweza kuendana na sera za kukuza biashara ili kuwashirikishawafadhili na wafuasi kwa pamoja.

Wafanyabiashara na wawekezaji wanaotazama uongozi huo wanaona chama kinachobeza matatizo yao na kuwafanya kuwa maadui. Kwa nini mfanyabiashara awekeze kwenye chama kinachomtukana?

Kwanini awekeze kwenye Chama ambacho kinahubiri shari badala ya heri.Kwanini Mfanyabiashara awekeze katika chama ambacho kutwa kuchwa kiko barabarani kina uhubiri chuki na mipasuko katika jamii?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...