WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya kukuza vipaji vya vijana kupitia uwekezaji katika sekta ya michezo na ujenzi wa miundombinu ya kisasa.
Akizungumza usiku wa kuamkia leo, Julai 31 2026 wakati tamasha la mchezo wa Masumbwi “Knockout ya Mama Season 9” liliofanyika katika ukumbi wa The super Dome Masaki jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amesisitiza mpango wa Serikali kujenga arena kubwa ya kisasa itakayokuwa kitovu cha matukio mbalimbali ya michezo na burudani nchini.
Amesema Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea kuunga mkono juhudi za vijana na wadau wa michezo nchini, huku Serikali ikiendelea kushirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika kuimarisha maendeleo ya michezo na kuibua vipaji.
.jpeg)




.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...