NA DENIS MLOWE, IRINGA


MBUNGE wa Jimbo la Isimani, Emanuela Mtatifikolo Kaganda, ametoa msaada wa mabati kwa waendesha bodaboda wa kijiji cha Itunundu kilichoko kata ya Itunundu jimbo la Ismani kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kijiwe chao cha kusubiri abiria, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zao za kuboresha mazingira ya kazi.

Akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo, Mtatifikolo alisema kuwa bodaboda ni kundi muhimu katika kuchochea uchumi na kutoa huduma za usafiri kwa wananchi, hivyo linastahili kupewa ushirikiano na mazingira bora ya kufanyia kazi.

Alieleza kuwa ujenzi wa kijiwe hicho utawasaidia waendesha bodaboda kupata sehemu salama na yenye staha ya kusubiri wateja, sambamba na kuimarisha mpangilio wa shughuli zao.

Mbunge huyo aliwataka wanufaika kuhakikisha wanatumia mabati hayo kwa lengo lililokusudiwa na kukamilisha ujenzi wa kijiwe hicho kwa wakati, huku akisisitiza umuhimu wa kutunza miundombinu hiyo mara baada ya kukamilika.

Kwa upande wao, waendesha bodaboda walimshukuru Mbunge huyo kwa msaada alioutoa, wakisema utachangia kwa kiasi kikubwa kukamilisha ujenzi wa kijiwe hicho na kuboresha mazingira yao ya kazi pamoja na huduma wanazozitoa kwa wananchi.

Walisema kuwa kutokana na joto kali la tarafa ya Pawaga ambapo inapatikana kijiji cha Itunundu msaada huo utasaidia kuepukana na hali hiyo kitu ambacho mbunge amejitoa kwa lengo la kusaidia vijana.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...