Polisi kata na watendaji wa kata zilizopo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kuratibu na kufanya doria za kutosha kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi ili kudumisha amani, utulivu na usalama uliyopo Kwenye kata zao. 

Wito huo umetolewa Julai 22, 2026 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Kaster Ngonyani katika kikao kazi kilicho wakutanisha Polisi Kata na watendaji wa kata zote zilizopo Wilayani Mpanda kilichofanyika Ukumbi wa Polisi Kantini Manispaa ya Mpanda.

Katika kikao hicho, kimewataka Polisi kata na watendaji kata kuhainisha maeneo korofi Kwenye kata zao na kuweka mikakati ya pamoja katika kufanya doria za kutosha kupitia vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na kutoa elimu kwa vikundi hivyo juu ya namna bora ya ufanyaji doria ikiwemo mbinu  matumizi ya nguvu za kadri na ukamataji salama bila kuleta madhara kwa wakamataji wa watuhumiwa wa uhalifu na kuwafikisha vituo .

Naye Mkuu wa Polisi Jamii Mkoa wa Katavi Mrakibu wa Polisi (SP) John Mwaipungu amewataka watendaji kata na Polisi kata hao kuendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wananchi ikiwemo namna bora ya kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na kudhibiti wizi kwa njia ya mitandao kwa kujenga tabia ya kupiga simu kabla ya kutuma pesa ili kuhakiki endapo namba wanazozitumia pesa wanazitambua. 

Aidha Mtendaji kata ya Ibindi Moses Mihayo amelipongeza Jeshi la Polisi kwa kuendelea kudumisha amani na utilivu inayoonekana katika maeneo yao pamoja na kuzidi kuwa karibu na wananchi kupitia Polisi kata na kuliomba Jeshi la Polisi kuendelea kufanya doria na misako ya mara kwa mara ili kutokomeza kabisa matukio ya kihalifu na wahalifu Kwenye makazi yao.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...