Na Pamela Mollel Arusha,
Waandishi wa habari wametakiwa kuongeza matumizi ya ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika kuwapa wananchi taarifa sahihi kuhusu namna fedha na rasilimali za umma zinavyotumika nchini
Wito huo umetolewa na Mkaguzi wa Nje wa Mkoa wa Arusha, Valence Rutakyamirwa, wakati wa warsha maalumu iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ya Tanzania (NAOT) kwa wanachama wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC)
Rutakyamirwa anasema ripoti za ukaguzi zina nafasi kubwa katika kuibua changamoto zilizopo kwenye usimamizi wa fedha za umma, utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uzingatiaji wa sheria katika taasisi za serikali
Anasema jukumu la ukaguzi halilengi pekee kubaini makosa, bali pia kusaidia taasisi za umma kujenga mifumo bora ya usimamizi, kuongeza uwajibikaji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma zinazostahili
“Waandishi wa habari wana nafasi muhimu ya kuzifanyia kazi ripoti hizi kwa kuzichambua, kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo na kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya fedha za umma,” anasema Rutakyamirwa.
Ameeleza kuwa katika kaguzi mbalimbali, NAOT imekuwa ikibaini changamoto katika maeneo ya manunuzi ya umma, usimamizi wa miradi ya maendeleo, utekelezaji wa mikataba na matumizi ya rasilimali za serikali
Kwa upande wake, Mchumi Mwandamizi kutoka Ofisi ya CAG, Emmanuel Lazaro, anasema taasisi hiyo inaendelea kuboresha mifumo yake ya ukaguzi kwa kutumia teknolojia za kisasa na mbinu mpya ili kuongeza ufanisi wa kazi
Anasema mpango mkakati wa NAOT unaendana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 kwa kuzingatia kuimarisha uwajibikaji, utawala bora na mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa
Aidha, Lazaro ametangaza mpango wa kuanzisha tuzo maalumu kwa waandishi wa habari watakaofanya kazi bora za uchunguzi zinazosaidia kuibua changamoto katika miradi ya maendeleo, matumizi ya fedha za umma na utekelezaji wa mapendekezo ya ukaguzi.
Hatua hiyo inalenga kuhamasisha uandishi wa habari unaochochea uwazi, uwajibikaji na usimamizi bora wa rasilimali za taifa.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...