Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imewasihi wadau wa ununuzi wa umma na wananchi kwa ujumla kutembelea banda la Mamlaka ya Rufani kupata uelewa juu ya majukumu na huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo hususan matumizi ya Moduli ya kupokea na kushughulikia malalamiko na rufaa katika mfumo wa NeST.


Wito huo umetolewa na Mkuu wa Sehemu ya Huduma za Sheria PPAA, Bi. Agnes Sayi kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando. Bi Sayi alitoa wito huo leo tarehe 01 Julai, 2026 katika Banda la Wizara ya Fedha Jijini Dar es Salaam kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba). 

Pamoja na mambo mengine, PPAA katika maonesho hayo inatoa elimu kuhusu uamuzi juu ya rufaa zinazotokana na mchakato wa ununuzi wa umma, uamuzi juu ya rufaa zinazotokana na kufungiwa kushiriki katika michakato ya ununuzi wa umma pamoja na uamuzi juu ya malalamiko yanayotokana na kushindwa kwa Afisa Masuuli kutoa uamuzi ndani ya muda uliowekwa.

“Maeneo mengine yanayotolewa elimu ni uamuzi juu ya malalamiko baada ya mkataba wa ununuzi kuanza kutekelezwa, uamuzi juu ya maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha rufaa nje ya muda uliowekwa, uamuzi juu ya maombi ya utekelezaji wa amri ya Mamlaka ya Rufani, uamuzi juu ya maombi ya kufuta uamuzi uliotolewa bila kusikiliza upande mwingine (Ex Parte decision) na uamuzi juu ya maombi ya kurejesha rufaa,” amesema Bi. Sayi

Maonesho hayo yameanza tarehe 28 Juni yataendelea hadi 13 Julai 2026 katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es Salaam. Aidha, Taasisi mbalimbali za Umma zimeshiriki maonesho hayo kwa lengo la kuonesha huduma wanazotoa kwa wananchi kwa kaulimbiu: Maonesho ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Fahari ya Tanzania.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...