NA DENIS MLOWE, IRINGA
MCHEZAJI wa Yanga SC na Timu ya Taifa ya Tanzania, Clement Mzize, ametangaza rasmi kufanyika kwa tamasha la hisani la "Washike Mkono" litakalofanyika Julai 12 katika Uwanja wa Samora mkoani Iringa, likiwa na lengo la kukusanya fedha za kusaidia makundi yenye mahitaji maalumu pamoja na kuhamasisha mshikamano kupitia michezo na burudani.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mzize alisema tamasha hilo ni mwendelezo wa juhudi zake za kurudisha kwa jamii kile alichojaliwa, huku akisisitiza kuwa kaulimbiu ya "Washike Mkono" inalenga kuwafikia wananchi wenye uhitaji kupitia sekta mbalimbali.
Alisema katika tamasha hilo bodaboda 100 watanufaika kwa kupewa mafuta, helmeti na reflector, huku msaada mwingine ukielekezwa kwenye shule kwa kujenga vyoo na hospitali kwa kutoa vifaa vya tiba ikiwemo mashine ya ultrasound.
Mzize aliwashukuru wadhamini mbalimbali waliowezesha maandalizi ya tamasha hilo, akiwemo GSM, Asas, Master Lim, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Jeshi la Polisi pamoja na wadau wengine waliotoa ushirikiano.
Alisema tiketi ya kuingia ni shilingi 3,000 pekee na kwamba kila tiketi itanunuliwa ni mchango wa moja kwa moja kwa ajili ya kuwasaidia watu wenye mahitaji.
"Tunawaomba wana Iringa na Watanzania kwa ujumla wajitokeze kwa wingi ukitoa shilingi 3,000 unakuwa sehemu ya kuwashika mkono wale wenye uhitaji lengo letu si burudani pekee bali kugusa maisha ya watu," alisema Mzize.
Mzize alisema kuwa mbali na mchezo wa hisani, tamasha hilo litakuwa na burudani mbalimbali zikiwemo muziki wa wasanii, michezo ya watoto, mechi za veterani pamoja na fursa kwa mashabiki kupiga picha na nyota wa soka watakaoshiriki.
Mzize alisema mastaa kadhaa wa soka wamethibitisha kushiriki, akiwemo Feisal Salum, Maxi Nzengeli, Bakari Mwamnyeto, Denis Nkane, Kibwana Shomari, Lomalisa Mutambala pamoja na wachezaji wengine wengi wa ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake, mchezaji Oscar Evaristo anayekipiga katika klabu ya Port Fouad ya nchini Misri alisema amefurahia kushirikiana na Mzize katika tamasha hilo kwa lengo la kuwasaidia wenye mahitaji na wakati huohuo kutoa nafasi kwa vipaji vya soka vya Iringa kuonekana.
Oscar alisema kikosi chake kitakuwa na nyota mbalimbali ambao hakutaka kuwataja wote mapema ili kutoa nafasi ya mashabiki kupata mshangao siku ya tamasha, huku akibainisha kuwa baadhi ya wachezaji wa Iringa watapewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao mbele ya wadau wa soka.
Naye Afisa Utamaduni na Michezo Mkoa wa Iringa, Steven Sanga, alisema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Mzize Foundation kuhakikisha maandalizi yote yanakamilika kwa wakati.
Alisema maandalizi muhimu yamekamilika, ikiwemo upatikanaji wa uwanja, huduma za kwanza, uratibu wa utoaji damu na ushirikiano wa taasisi mbalimbali za serikali ngazi ya mkoa na wilaya.
Sanga alibainisha kuwa tamasha hilo litakuwa zaidi ya mchezo wa soka kwa kuwa litatoa fursa ya burudani, kujifunza kutoka kwa wachezaji wa kiwango cha juu na kuimarisha mshikamano wa wananchi kupitia michezo.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James huku waandaaji wakitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani na wakati huohuo kuchangia kuwasaidia watu wenye mahitaji kupitia tamasha la "Washike Mkono".

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...