Na Mwandishi Wetu
TANZANIA imesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya nchi za Afrika katika kuimarisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia hususan kwenye vifaa visivyotumika kwa uchunguzi wa kitabibu, ili kuongeza ufanisi wa matumizi ya teknolojia hiyo katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Hayo ameyasema Mjumbe wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk, Amos Nungu, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya usalama wa mionzi ya nyuklia kwenye vifaa visivyo vya uchunguzi wa kimatibabu uliowakutanisha washiriki i 35 kutoka nchi 25 za Afrika.
Dkt. Nungu amesema mafunzo hayo ya wiki nzima yameandaliwa na Shirika la Kimataifa la ya Atomu (IAEA) na yamekuwa fursa muhimu kwa nchi za Afrika kujifunza kutoka kwa wataalamu wa kimataifa pamoja na kubadilishana uzoefu kutokana na hatua mbalimbali za maendeleo ambazo kila nchi imefikia katika matumizi ya teknolojia ya nyuklia nje ya sekta ya tiba.
Dkt.Nungu amesema kuwa washiriki wanapata nafasi ya kusikiliza mawasilisho kutoka kwa kila nchi kuhusu mafanikio, changamoto na mikakati yao, jambo linalowezesha kujifunza kutoka kwa wenzao na kufanya tathmini ya maendeleo yao. Aidha, aliwataka washiriki wa Tanzania kutumia vyema fursa hiyo kwa kujifunza kutoka kwa wataalamu waliotoka mataifa yenye uzoefu mkubwa, ikiwemo Ureno, pamoja na wenzao wa Afrika.
Dkt. Nungu ameongeza kuwa ushirikiano huo utaisaidia Tanzania na nchi nyingine za Afrika kuimarisha usalama wa mionzi ya nyuklia, kuboresha mifumo ya udhibiti na kuongeza matumizi ya teknolojia ya nyuklia katika sekta mbalimbali za maendeleo kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya usalama.
Nae Mtafiti na Mkaguzi wa Usalama wa Mionzi wa TAEC Elisha Edmund Amesema mafunzo hayo yamelenga kuimarisha uelewa na uwezo wa wataalamu katika usimamizi salama wa matumizi ya teknolojia hiyo.
Amesema mafunzo yataisaidia shughuli za ufuatiliaji na kukabiliana na uwezekano wa kuwepo kwa vifaa au nyenzo za mionzi ambazo zinaweza kuhatarisha usalama.
Edmund amesema mafunzo hayo watajadili changamoto mbalimbali ili kulinda wafanyakazi, wananchi na mazingira.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...