Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC), Samuel A. Mshote, amesema matumizi ya mbolea nchini yameendelea kuongezeka na kuchangia kupungua kwa changamoto kwa wakulima pamoja na kuimarika kwa usalama wa chakula nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Julai 5, 2026, Mshote alisema hali ya uzalishaji wa chakula imeendelea kuimarika, ambapo kwa sasa Tanzania inajitosheleza kwa chakula kwa zaidi ya asilimia 124, na mafanikio hayo yanatokana na juhudi za Serikali katika kuhakikisha matumizi ya mbolea yanaongezeka nchini, hali iliyosaidia kuongeza tija katika sekta ya kilimo.

Mshote alisema matumizi ya mbolea yameongezeka kutoka takribani tani 360,000 kwa miaka mitatu iliyopita hadi zaidi ya tani milioni 1.2 kwa mwaka kwa mbolea aina mbalimbali zinazotumika na wakulima nchini, elimu kuhusu matumizi ya mbolea kwa wakulima imeendelea kuimarika, jambo ambalo linatarajiwa kuongeza zaidi tija katika uzalishaji wa mazao kadri muda unavyosonga mbele.

Aidha, alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha matumizi ya mbolea yanafikia kilo 50 kwa hekta, ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Umoja wa Afrika kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, lenye lengo la kuongeza uzalishaji wa kilimo, amebainisha kuwa ifikapo mwaka 2030, Tanzania inatarajia kufikia malengo ya uzalishaji yaliyowekwa kupitia azimio hilo ili kuimarisha zaidi sekta ya kilimo.

Kuhusu upatikanaji wa mbolea, alisema Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imeanza kutekeleza mipango mbalimbali ambapo tani 70,000 zimeingizwa nchini kwa ajili ya matumizi ya wakulima, pia tani 30,000 za mbolea za kupandia zinatarajiwa kupokelewa wiki ijayo, ambazo zitasambazwa kwa wakulima ili kuanza maandalizi ya msimu mpya wa kilimo.

Aidha, alieleza kuwa Serikali imeagiza tani 40,000 za mbolea aina ya Urea ambazo zinatarajiwa kupokelewa mwezi ujao kwa ajili ya kuingizwa sokoni na kusaidia wakulima katika hatua za kukuzia mazao.'



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...