Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Mwigulu Nchemba amekagua maandalizi ya siku ya mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali Mtumba Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza mara maada ya kushuhudia majaribio ambayo yamefanywa na vikosi vya ulinzi na usalama amesema kuwa mpaka sasa mambo yanaenda vizuri na kupongeza maandalizi hayo.
"Nimekuja kujionea hatua ya maandalizi yanayoendelea kabla ya tukio letu kubwa na la kihistoria ambalo litafanyika tarehe 25/7/2026,, nikiri nimeridhishwa na maandalizi kufuatia taarifa ambayo tumepokea na kile ambacho tumejionea,,,.
Hapo awali Waziri wa Mambo ya Ndani kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi Mhe,Patrobas Katambi akisoma taarifa ya maandalizi amesema katika ya siku ya mashujaa tayari vipo vikundi mbalilimbali kutoka katika vyombo vya ulinzi na usalama.
Ameongeza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama Mhe.Dkt Samia Hassan kwa maelekezo yake mahususi kwa ajiri ya kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi.
" Tunawahakikishia Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wako salama na kwa wageni wanaokuja kwa kufuata utaratibu nao wako salama,,.
Katika tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule na wakuu wa vyombo ulinzi na Usalama wa Mkoa huu.








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...