Na Janeth Raphael -MichuziTv
Katika hatua ya kuimarisha ubora wa elimu nchini, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) umetangaza kuimarisha na kupanua mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo viongozi wa sekta ya elimu ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shule na taasisi za elimu.
Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 6, 2026, jijini Dodoma, Mtendaji Mkuu wa ADEM, Dkt. Maulid Maulid, amesema taasisi hiyo inaendelea kutekeleza mkakati wa kuwapa viongozi wa elimu maarifa na ujuzi wa kisasa unaowawezesha kukidhi mahitaji ya sekta ya elimu inayobadilika kwa kasi.
Amesema mafunzo hayo yanawahusisha wakuu wa shule, walimu wakuu, maafisa elimu wa kata, halmashauri na mikoa, pamoja na wathibiti ubora wa shule, kwa lengo la kuongeza uwajibikaji, kuimarisha utawala bora na kuboresha usimamizi wa rasilimali za elimu.
Kwa mujibu wa Dkt. Maulid, tangu kuanzishwa kwa programu ya Stashahada ya Uongozi, Usimamizi na Utawala katika Elimu (DELMA), wahitimu 8,599 wamehitimu kati ya mwaka 2002 na 2025. Aidha, wahitimu 2,263 wamekamilisha Stashahada ya Uthibiti Ubora wa Shule (DSQA) tangu mwaka 2016.
Katika mwaka wa masomo 2025/2026 pekee, ADEM ilidahili wanafunzi 2,016, huku wengi wao wakijiunga na programu ya DELMA, hatua inayoonesha kuongezeka kwa mahitaji ya mafunzo ya uongozi wa elimu nchini.
Dkt. Maulid amesema mafunzo hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha utendaji wa viongozi wa elimu, kuimarisha matumizi ya TEHAMA katika usimamizi wa shule na kuongeza uwajibikaji katika utoaji wa huduma za elimu.
Ameeleza kuwa kupitia Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi (BOOST), ADEM imepokea zaidi ya shilingi bilioni 16 kwa ajili ya kutoa mafunzo ya uongozi kwa viongozi wa elimu katika kipindi cha miaka mitano.
Kupitia mradi huo, zaidi ya walimu wakuu 17,817, waratibu elimu wa kata zaidi ya 3,900 pamoja na maafisa elimu wa wilaya na mikoa tayari wamenufaika na mafunzo hayo, yanayolenga kuboresha huduma za elimu katika shule za umma.
Mbali na mafunzo, ADEM inaendelea kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu maboresho ya sera za elimu, huku ikipanua ushirikiano na taasisi za ndani na nje ya nchi ili kuimarisha matumizi ya teknolojia na ubora wa mafunzo.
Kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ADEM imejipangia kuongeza udahili wa wanafunzi wa mafunzo ya muda mrefu hadi 3,500, kuanzisha programu mpya za mafunzo, kuboresha miundombinu ya kampasi zake za Bagamoyo, Mbeya na Mwanza pamoja na kupanua matumizi ya TEHAMA.
Hatua hizo zinatarajiwa kuongeza uwezo wa viongozi wa elimu kusimamia mageuzi ya sekta hiyo na kuchochea utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga mfumo wa elimu wenye ushindani na unaokidhi mahitaji ya maendeleo ya taifa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...