Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli, amewapongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa mchango wake mkubwa katika utoaji wa huduma za ujenzi na usimamizi wa majengo ya Serikali, akieleza kuwa taasisi hiyo imekuwa mshirika muhimu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya wizara.
Mweli ameyasema hayo Agosti 6, 2026, baada ya kutembelea banda la TBA katika Maonesho ya Kilimo Nanenane Kitaifa yanayoendelea jijini Dodoma, amesema Wizara ya Kilimo imefanya kazi nyingi kwa kushirikiana na TBA, ikiwemo usimamizi wa ujenzi wa maghala, usanifu wa jengo la wizara pamoja na usimamizi wa miradi hiyo kwa weledi na ubora wa hali ya juu.
Ameeleza kuwa TBA imeendelea kujidhihirisha kama taasisi yenye uwezo wa kutoa huduma za ujenzi na usimamizi wa majengo zinazokidhi viwango, si kwa taasisi za serikali pekee bali pia kwa sekta binafsi, jambo linalochangia kuimarisha miundombinu ya maendeleo nchini.
Mweli amewahimiza wananchi na wadau wanaotembelea Maonesho ya Nanenane kuhakikisha wanapita katika banda la TBA lililopo eneo la Private Sector Pavilion, ili kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na wakala huo pamoja na kupata taarifa kuhusu fursa zilizopo katika sekta ya ujenzi na usimamizi wa majengo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...