Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Katikati), akipewa maelezo kuhusu huduma mbalimbali za kibenki zinazotolewa na Benki ya Absa Tanzania, alipotembelea banda la benki hiyo, wakati wa maonesho ya 32 ya Kimataifa ya Wakulima ya Nane Nane, yaliyohitimishwa jana kwenye Viwanja vya Dk. John Samuel Malecela, Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Mwilongo Msungu (wa pili kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma za kibenki zinazotolewa na benki hiyo kwa mkazi wa Dodoma, Pius Killo, alipofika katika banda la benki hiyo, wakati wa maonesho ya 32 ya Kimataifa ya Wakulima ya Nane Nane, yaliyomalizika jana kwenye Viwanja vya Dk. John Samuel Malecela, Mkoani Dodoma. Kushoto ni Meneja wa benki hiyo Mkoani Dodoma, Bw. Deogratias Luena na wa tatu kushoto ni Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi.
Meneja wa Benki ya Absa Mkoani Dodoma, Bw. Deogratias Luena (katikati), akitoa maelezo kuhusu huduma za kibenki zinazotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la benki hiyo, wakati wa maonesho ya 32 ya Kimataifa ya Wakulima ya Nane Nane, yaliyomalizika jana, kwenye Viwanja vya Dk. John Samuel Malecela, Mkoani Dodoma.Mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Absa Mkoani Dodoma, Bw. Emmanuel Basharasha, akitoa maelezo kuhusu huduma za kibenki zinazotolewa na benki hiyo kwa baadhi ya watembeleaji katika banda la benki hiyo, wakati wa maonesho ya 32 ya Kimataifa ya Wakulima ya Nane Nane, kwenye Viwanja vya Dk. John Samuel Malecela, Mkoani Dodoma jana.
Ofisa Mauzo wa Benki ya Absa Tawi la Dodoma, Bw. Gabriel Mlaga (kulia), akimpiga picha kwa ajili ya kufungua akaunti mpya ya mmoja ya wateja waliofika katika banda la benki hiyo, wakati wa maonesho ya 32 ya Kimataifa ya Wakulima ya Nane Nane, kwenye Viwanja vya Dk. John Samuel Malecela, Mkoani Dodoma jana.
Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi ya Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Mwilongo Msungu (wa pili kulia), akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa zinazotokewa na benki hiyo kwa Ofisa Mwandamizi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB), Dk. John Joseph (wa pili kushoto), alipotembelea banda la benki hiyo, wakati wa maonesho ya 32 ya Kimataifa ya Wakulima ya Nane Nane yaliyohitimishwa jana kwenye Viwanja vya Dk. John Samuel Malecela, Mkoani Dodoma.Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi ya Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Mwilongo Msungu (katikati), Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa benki hiyo, Bi. Abigail Lukuvi (wa pili kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa Absa tawi la Dodoma, wakipiga picha ya pamoja katika banda lao benki, wakati wa maonesho ya 32 ya Kimataifa ya Wakulima ya Nane Nane, kwenye Viwanja vya Dk. John Samuel Malecela, Mkoani Dodoma.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...