Waswahili husema Chanda chema huvikwa pete msemo ambao umedhihirika siku ya mnyama “Simba Day “ baada ya klabu hiyo kumtunuku tuzo Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Abdul-Razaq Badru kutokana na mchango wake mkubwa wa kuunganisha utalii na michezo.
Kamishna Badru amekabidhiwa tuzo hiyo kutokana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kukubali na kushiriki kikamilifu maadhimisho ya wiki ya simba ambapo mamlaka ilitumia fursa hiyo kutangaza shughuli zake za uhifadhi na utalii na kukaribisha wadau mbalimbali kurudi nyumbani Ngorongoro
Dhamira ya Kamishna Badru ni kuhakikisha kuwa utalii wa Ngorongoro na michezo unafungamanishwa sambamba ambapo tarehe 13 Julai,2026 mamlaka hiyo na klabu ya Simba ziliafikiana kushirikiana katika tukio hilo lenye mamilioni ya watazamaji ndani na nje ya nchi ambalo uzinduzi wake ulifanyika tarehe 1 agosti, 2026 ndani ya Kasoko ya Ngorongoro.
“Chapa hizi mbili kubwa kimataifa zinaafikiana katika jambo hili kwa kuwa tunataka kutangaza utalii wa vivutio vilivyopo Ngongoro ndani na nje ya nchi na tuna uhakika tutafanikiwa kutokana na ukubwa wake na kusaidia dhamira ya Serikali kuongeza wageni wengi zaidi wanaotembelea Ngorongoro ambayo ni kivutio namba moja Afrika kwa mwaka 2023 na 2025 ”.alisema Kamishna Badru.
Kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Klabu ya Simba kukamilisha tukio hilo jana tarehe 8, Agosti 2026 ni kama wamepiga bao la kusigino kutokana na maelfu ya watu kushiriki na kuridhika kwa mafanikio ya “Simba Day”.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...