Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), imefanya ziara ya ukaguzi katika mradi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko, kwa lengo la kujionea hatua ya utekelezaji wa mradi, kukagua miundombinu na maandalizi yaliyofanyika kuelekea kuanza kwa matumizi ya bandari hiyo, pamoja na kutathmini fursa zitakazotokana na uwekezaji huo katika shughuli za uvuvi na uchumi wa buluu.

Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 20 Agosti 2026, ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Yunus D. Mgaya, ambapo Bodi hiyo imepata fursa ya kukagua maeneo mbalimbali ya bandari na kupata maelezo kuhusu hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya kuanza kwa shughuli zake.

Akizungumza baada ya ziara hiyo, Prof. Mgaya, amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo, akieleza kuwa kukamilika na kuanza kufanya kazi kwa Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko kutakuwa hatua muhimu katika kuimarisha sekta ya uvuvi nchini.

"Bandari hii ina nafasi kubwa katika kuongeza ufanisi wa shughuli za uvuvi, kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi, pamoja na kutoa fursa za ajira na biashara. Nawahimize wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kutumia fursa zilizopo katika Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko kwa kuwekeza katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na sekta ya uvuvi," aliongeza Prof. Mgaya

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa TAFICO, Dkt. Suleiman Kiula, ndc , amesema Shirika hilo linaendelea na mchakato wa kushirikisha sekta binafsi pamoja na wadau mbalimbali kuhakikisha bandari hiyo inaendeshwa kwa ufanisi, kwa kutoa huduma wezeshi kwa viwango bora na nafuu ili kuvutia Meli nyingi kutumia bandari hiyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Dkt. Kiula amesema TAFICO inaendelea kutekeleza mikakati ya kushiriki kikamilifu katika kuendeleza shughuli za uvuvi wa kisasa na ukuzaji viumbe maji, ikiwemo uwekezaji katika Meli za uvuvi wa bahari kuu, uanzishaji wa mashamba ya kufuga samaki, miundombinu wezeshi, pamoja na kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi.

"Kuanza kwa shughuli za Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko kutafungua fursa mbalimbali kwa wavuvi, wafanyabiashara na wawekezaji, huku kukiwa na matarajio ya kuongeza ajira na kuchochea shughuli za kiuchumi katika Wilaya ya Kilwa na maeneo mengine nchini," alieleza Dkt. Kiula.

Bandari ya Uvuvi Kilwa Masoko ni mradi wa kimkakati unaolenga kuimarisha shughuli za uvuvi nchini. Miundombinu ya bandari hiyo inajumuisha gati lenye urefu wa mita 315 la kuhudumia meli za uvuvi zaidi ya kumi kwa wakati mmoja, eneo la kuhifadhi samaki, mtambo wa kizalisha barafu na eneo la matengenezo ya meli, hatua inayolenga kuongeza ufanisi katika shughuli za uvuvi na mnyororo wa thamani wa mazao ya uvuvi.



























Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...