Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya wanafunzi 95 wa Kitanzania wameondoka nchini kuelekea India kuanza masomo ya elimu ya juu katika vyuo mbalimbali, ikiwa ni kundi la kwanza kati ya wanafunzi 198 wanaotarajiwa kwenda kusoma nchini humo kupitia Global Education Link mwaka 2026.

Wanafunzi hao wamechagua programu zinazohusiana na sayansi, teknolojia na taaluma zinazohitajika katika dunia ya sasa, zikiwemo Computer Engineering, Cyber Security, Artificial Intelligence, Civil Engineering, afya, sheria na biashara.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Global Education Link, Meneja wa Tawi la Dar es Salaam, Micky Musa, amesema kuondoka kwa wanafunzi hao ni sehemu ya mpango wa kuwaunganisha vijana wa Tanzania na fursa za elimu ya kimataifa.

“Zaidi ya wanafunzi 95 wanaondoka katika kundi hili la kwanza kuelekea India, lakini kwa mwaka huu tunatarajia wanafunzi 198 kwenda kusoma nchini India. Hili si kundi la mwisho kwa sababu bado tuna wanafunzi wengine wanaoendelea kukamilisha taratibu zao,” amesema Musa.

Amesema Global Education Link pia inaendelea kuwaandaa wanafunzi wapatao 185 wanaotarajiwa kuelekea China, huku wengine wakiwa katika maandalizi ya kwenda Malaysia, Marekani na Uingereza.

Musa amewataka vijana wenye ndoto ya kusoma nje ya nchi kufika katika ofisi za Global Education Link zilizopo Dar es Salaam, Dodoma, Zanzibar, Mwanza na Arusha kupata ushauri kuhusu uchaguzi wa vyuo, programu za masomo, udahili, visa na maandalizi ya safari.

Miongoni mwa wanafunzi walioondoka ni Alvin Andrew Munda, mwenye umri wa miaka 17, anayeelekea Lovely Professional University nchini India kusomea Computer Science, akilenga baadaye kujikita katika Cyber Security.

“Napenda mfumo wenye practical zaidi kuliko kusoma theory na kuandika mitihani pekee. Nataka nitumie elimu nitakayoipata kutengeneza suluhisho na baadaye nijikite katika Cyber Security kwa sababu usalama wa mtandao ni muhimu sana katika dunia ya sasa,” amesema.

Munda amesema Global Education Link imemsaidia katika mchakato mzima, kuanzia kupata chuo hadi kukamilisha maandalizi ya safari.

Naye mwanafunzi mwingine anayekwenda kusomea Computer Science na Artificial Intelligence amesema anatarajia kuwa mtaalamu wa data na teknolojia, akieleza kuwa AI imeanza kuwa sehemu muhimu katika benki, hospitali, biashara, serikali na sekta nyingine.

Kwa upande mwingine, mwanafunzi anayekwenda kusomea Bachelor of Business Administration na Bachelor of Laws amesema ana ndoto ya kuwa mwanasheria na mfanyabiashara mwenye mafanikio, huku akipongeza Global Education Link kwa kumsaidia katika visa processing, kupata chuo na maandalizi ya safari.

Wazazi waliowasindikiza watoto wao Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wameipongeza Global Education Link kwa kusimamia mchakato wa watoto wao kuanzia hatua za awali hadi siku ya safari.

Donald Kito, mzazi wa Isaac Donald Kito anayekwenda Lovely Professional University kusomea Diploma ya Civil Engineering, amesema familia yake ilifahamu huduma za Global Education Link kupitia matangazo na baada ya kuwasiliana nao walipata maelezo yaliyowapa imani ya kuendelea na mchakato.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...