Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwl. Protas Magesa amefanya kikao maalum na watumishi wastaafu wa CWT, ikiwa ni kuthamini mchango wa waasisi na watumishi wastaafu wa chama waliowahi kutumikia kwa nyadhifa mbalimbali.

Kikao hicho kimefanyika leo katika Ukumbi wa Royal Village, jijini Dodoma, kikiongozwa na Kaimu Katibu Mkuu wa CWT, Mwl. Magesa Protas Magesa, akiambatana na Kaimu Mwekahazina wa CWT, Mwl. James Asagwile, pamoja na viongozi wa CWT Mkoa wa Dodoma.

Chama cha Walimu Tanzania, CWT, kimeendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuthamini mchango wa watumishi wastaafu kwa lengo la kusikiliza ushauri, maoni na uzoefu wao kiutendaji kuhusu mustakabali wa chama na namna bora ya kuendelea kukijenga ili kiweze kuwahudumia wanachama kwa ufanisi zaidi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mwl. Magesa amesema uongozi wa sasa unaamini kuwa uzoefu wa watumishi wastaafu ni hazina muhimu katika kuimarisha utendaji wa chama na miongoni mwa vipaumbele vya uongozi wake ni kuboresha huduma kwa wanachama na kutatua changamoto zilizodumu kwa muda mrefu, ikiwemo kuanza kulipa madeni ya mkono wa kwaheri pamoja na mabati kwa wastaafu.

Mwl. Magesa amesisitiza kuwa anatambua mchango mkubwa wa watumishi hao, wengi wao wakiwa sehemu ya waasisi walioijenga CWT tangu kuanzishwa kwake zaidi ya miaka 30 iliyopita na ameahidi kuendeleza maono yao kwa kuhakikisha chama kinaendelea kuwa imara, chenye mshikamano na kinachotetea maslahi ya walimu kwa ufanisi pia ni sehemu ya juhudi za uongozi wa CWT .

Kwa upande wake, Kaimu Mwekahazina wa CWT, Mwl. James Asagwile, amesema waasisi wa chama wameweka msingi imara uliowezesha kuzalisha viongozi wengi wanaoendelea kulitumikia taifa kupitia CWT. pia mebainisha kuwa uongozi wa sasa utaendelea kusikiliza ushauri wao na kwamba uzoefu wa watumishi wastaafu ni nguzo muhimu katika kuendelea kuijenga CWT.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wastaafu, Mwl. Dauda Bilikesi ameishukuru Ofisi ya Katibu Mkuu kwa kuandaa kikao hicho, akisema hatua hiyo imeonesha kuthamini mchango wa waliolitumikia chama kwa miaka mingi na kwasasa wastaafu wana matumaini makubwa ya kuona CWT ikiendelea kukua na kuimarisha nafasi yake katika kutetea na kuzungumzia maslahi ya walimu nchini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...