JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kisarika wilayani Moshi, Nelson Mkenda (17), kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi mwenzake aitwaye Vicent Mmary, (17) wa shule ya Sekondari Kisarika, kidato cha tatu kwa kitu chenye ncha kali kifuani na kusababisha kifo chake.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, SACP Saimon Maigwa alisema kuwa, tukio hilo limetokea Agosti 28 mwaka huu majira ya saa tisa na robo alasiri huko katika shule ya Sekondari Kisarika, kitongoji cha Manushi, kijiji cha Ongomauru, Kata ya Uru Kaskazini, Wilaya ya Moshi.
Alisema kuwa, ulitokea ugonvi baina yao baada ya Marehemu kumtuhumu Mtuhumiwa kuiba vitu mbalimbali kwenye mabweni ya shule hiyo.
Mwanafunzi huyo alifariki dunia akiwa njiani kuelekea hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mawenzi kwa matibabu.
Uchunguzi wa kina unaendelea ili kukamilisha taratibu za kisheria na kumfikisha mtuhumiwa Mahakamani.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...