Na Dulla Uwezo
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 zinatarajia kuingia Mkoani Kagera Agosti 30, Mwaka huu zikitokea Mkoa wa Geita, zikipokelewa rasmi katika Wilaya ya Muleba na Viongozi wa Mkoa huo wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Kagera Kanali Yahya Ramadhani Kido.
Kwa Mujibu wa Taarifa iliyotolewa mbele na Wanahabari na Mkuu wa Mkoa Kagera Kanali Kido, amesema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa Mkoani humo utatembelea miradi 54 yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 23.07 ikiwemo miradi ya Serikali, Binafsi (wawekezaji) pamoja na ili inayotekelezwa kwa Kushirikiana na Nguvu ya Jamii.
Aidha Kanali Kido ameongeza kuwa kati ya Miradi 54, Miradi 25 itawekewa Mawe ya Msingi, Miradi 5 itafunguliwa, Miradi 11 itazinduliwa, na Miradi 13 Itatembelewa na Kukaguliwa. Miradi hiyo ni pamoja na Miradi ya Maji, Afya, Elimu, Miundo Mbinu, Maendeleo ya Vijana, Nishati, Mazingira wezeshi kwa wawekezaji pamoja na Uhifadhi Mazingira.
Pamoja na hayo Mkuu wa Mkoa Kagera Kanali Kido ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa Wingi kule kote ambapo Mwenge utapita, maeneo ya miradi pamoja na maeno ya Mikesha ya Mwenge, huku Mwenge wa Uhuru ukiwa na Umebeba Ujumbe wa Masuala ya UKIMWI, Malaria, Dawa za Kulevya, Masuala ya Lishe, Rushwa Sambamba na Kauli mbiu isemayo "Tanzania ni yetu sote, tushikamane kwa pamoja kuleta maendeleo."



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...