Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar, Ndg. Abdi Mahamoud Abdi, amewataka viongozi na watendaji wa chama katika ngazi zote kufanya kazi kwa bidii, mshikamano na ushirikiano wa pamoja ili kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinaendelea kupata matokeo chanya katika utekelezaji wa majukumu yake.

Ndg. Abdi ameyasema hayo leo, Agosti 17, 2026, katika ukumbi wa Jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Zanzibar, wakati akizungumza katika kikao cha pamoja kilichowakutanisha viongozi na watendaji wa CCM, Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuiya ya Wazazi pamoja na watendaji wa Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.

Amesema kila mtendaji wa chama ana jukumu la kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kwa bidii, uadilifu na kwa kuzingatia wajibu aliopewa katika kitengo chake, huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha ushirikiano na watendaji wenzake.

Ndg. Abdi amesema mafanikio ya chama yanategemea kwa kiasi kikubwa namna viongozi na watendaji wake wanavyoshirikiana katika kutekeleza majukumu yao, hivyo amewataka kuacha kufanya kazi kwa misingi ya mtu mmoja mmoja na badala yake kujenga utamaduni wa kufanya kazi kwa pamoja.

Aidha, Naibu Katibu Mkuu huyo amewatoa hofu watendaji wa chama kuhusu masuala ya maslahi yao, akisisitiza kuwa ataendelea kusimamia kikamilifu maslahi yao ili kuwawezesha kuwa na mazingira bora yatakayowapa motisha ya kufanya kazi kwa bidii na kwa ufanisi zaidi.

Amesisitiza kuwa watendaji wanapaswa kutumia nafasi zao kwa kutekeleza majukumu ya chama kwa ufanisi, huku wakilinda umoja, mshikamano na misingi ya Chama Cha Mapinduzi.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...