Hatimaye ile Derby ya kibabe iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ya Ngao ya Jamii imefika. Je Ni Simba au Yanga kuondoka na pointi 3?. Tengeneza jamvi lako la uhakika na uwe mshindi sasa.

Jumatano tutashuhudia mtanange mkali wa Ngao ya Jamii kati ya Simba dhidi ya Yanga kule Zanzibar katika Dimba la New Aman Complex huku vijana wa Manqoba wakiingia kama mabingwa watetezi wa Kombe hili.

Huu ni mchezo wa kwanza wa ushindani wa msimu mpya, ushindi utakuwa na maana kubwa kwa upande utakaoibuka na Kombe hili, kwani utatoa ujumbe wa mapema kuhusu nguvu na utayari wa timu kuelekea msimu wa 2026/27.

Klabu hii ambayo ina makazi yake pale mitaa ya Twiga na Jangwani ambao ni mabingwa mara tano mfululizo kwenye ligi wanapewa nafasi kubwa ya kufanya vyema kwenye mechi hii kutokana na uimara ambao wameendelea kuuonesha ndani ya misimu hii. Manqoba Mngqithi ndiye ambayo amekabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi hiki na kuleta mafanikio.

Lakini pia Meridianbet inakwambia tengeneza mkwanja kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Ikumbukwe kuwa Manqoba ni kocha waliyemtoa Afrika Kusini ambaye amevinoa vilabu mbalimbali akihudumu katika nafasi mbalimbali ikiwemo Mamelodi Sundwons, alikuwa kocha mkuu wa timu ya Lamontville Golden Arrows kabla hajajiunga na Yanga. Ni kocha ambaye anatarajiwa kufanya vyema kwenye ligi kuu ya Tanzania hasa kwenye mitaa ya Jangwani.

Huku Simba wao wamekuwa na misimu migumu hasa baada ya kuendelea kukosa mataji hasa ya ligi kuu, lakini sasa chini ya kocha mkuu Steve Barker ambaye amejiunga na klabu hiyo akitokea Stellenbosch ya Afrika Kusini na anatarajiwa pia kuleta upinzania mkubwa kabisa kwenye msimu huu. Meridianbet inakwambia mechi hii ina machaguo zaidi ya 1000.

Jambo zuri ni kwamba hii ni mechi ambayo inakutanisha timu mbili ambazo zinanolewa na makocha ambao wanatoka Afrika Kusini hivyo mbinu ndio zinaweza kuamua nani ataibeba Ngao ya Jamii msimu huu.

Mechi 5 za mwisho walizokutana kati ya Simba dhidi ya Yanga Yanga ameshinda mechi 3 na Simba ametoa sare 1 na ameshinda mechi 1, hivyo vijana hawa wa Manqoba ndio wana nafasi nzuri ya kupata matokeo mazuri kutokana na kikosi bora ambacho wanacho.

Timu zote zimefanya usajili mzuri huku upande wa Yanga ameongeza wachezaji kama Peter Shalulile aliyekuwa Mamelodi, Cheikh Ibrahima Touré, Albert Kangwanda kutoka Zambia, Mouhamed Komara kutoka Ivory Coast na wengine wengi ambao wamekuja kuongeza nguvu kikosini hapo.

Lakini bado kwenye klabu hiyo kuna wachezaji tishio na wa kuchungwa Pacome, Nzengeli, Abuya Okelo na wengine huku wakiwa na kipa mzuri Diara. Je Nani kuondoka na ushindi siku ya leo?. Odds Kubwa zipo kwenye mechi hii sasa.

Simba wao baadhi ya wachezaji ambao wamewaongeza ni pamoja na Ibrahim Doumbia kutoka Mali, Keletso kutoka Sekhukhune United, Ibraheem Jabaar kutoka Stellenbosch, Nathaniel Chilambo kutoka Azam , Kelvin Nashon ambao nao wamekuja kuungana na wachezaji waliopo kusaka mataji.

Wekundu wa Msimbazi, wana wachezaji wakuchungwa wakiwemo, Mpanzu, Chama, Gueye, Kagoma na wengine wengi. Hivyo kwa ujumla timu ambayo itajiandaa vyema ndio ambayo itaondoka na ushindi. Jisajili hapa na ubeti leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...