Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza umuhimu wa madrasa kuendelea kutoa elimu bora ya dini, sambamba na kuwajengea watoto uelewa wa mafundisho wanayopokea, maadili mema na misingi sahihi ya maisha ya Kiislamu.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 07 Agosti 2026, alipojumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa iliyosaliwa katika Msikiti Al Aqswaa uliopo Kiboje, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

Amesema elimu ya madrasa ina nafasi kubwa katika kumjenga mtoto kielimu, kiimani na kimaadili, hivyo ni muhimu watoto wasifundishwe kusoma pekee, bali waelekezwe pia kuelewa maana na tafsiri ya mafundisho wanayojifunza.

Aidha, ameeleza umuhimu wa kuendelea kuwaandaa na kuwaendeleza walimu wa madrasa ili wawe na uwezo wa kufundisha kwa ufanisi na kuwajengea watoto uelewa mpana wa elimu ya dini wanayopokea.

Halikadhalika, Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa Serikali, viongozi wa dini, wazazi na jamii kwa ujumla kuendelea kushirikiana katika kuimarisha elimu ya madrasa na kushughulikia changamoto zinazokabili taasisi hizo.

Wakati huo huo, Rais Dkt. Mwinyi amefungua rasmi Madrasa ya Fatma, iliyopo Kiboje Mkwajuni, na kueleza matumaini yake ya kuona madrasa hiyo ikitoa mchango mkubwa katika elimu na malezi ya watoto.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...