Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Mawakala wa Forodha Tanzania (TAFFA) wamekuja na Mfumo wa Tanzania Customs Agent Management System (T-CAMS) unaoshirikisha TRA ikiwa ni sehemu ya mageuzi ya kidigitali yanayojenga uwazi, ufanisi na ushindani katika sekta ya uwakala wa forodha nchini.
Taarifa iliyotolewa na TAFFA kwa vyombo vya habari leo Agosti 7,2026 imesema mfumo huo unalenga kuleta uwazi katika malipo, kulinda heshima na maslahi ya mawakala wa forodha, kurahisisha huduma kwa waagizaji wa mizigo na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Imeongeza kwamba mfumo huo pia ni utekelezaji wa tangazo katika gazeti la serikali (GN) namba 83 la Machi, 2026 lililotolewa na shirika la uwakala wa meli Tanzania (TASAC).
Kuhusu changamoto zilizokuwepo TAFFA imesema kwa miaka mingi, sekta ya uwakala wa forodha ilikabiliwa na changamoto kadhaa. “Kwanza, kulikuwa na migogoro ya malipo kati ya mawakala na waagizaji wa mizigo. Mara nyingi wakala alikamilisha kazi lakini malipo yalicheleweshwa au hayakulipwa kabisa.
“Pili, kulikuwepo ushindani usio wa haki ambapo baadhi ya mawakala walishusha gharama za huduma kwa kiwango kisichoendana na ubora wa kazi ili kupata wateja.Tatu, mfumo usio rasmi wa malipo uliifanya Serikali kushindwa kupata taswira sahihi ya mapato yanayotokana na sekta hii, jambo lililofungua mianya ya ukwepaji wa kodi na kupunguza uwazi.”
Kuhusu T-CAMS ni mfumo wa kidijitali unaounganisha malipo ya kodi za forodha na ada ya wakala katika utaratibu mmoja ulio wazi na unaofuatilika.
Kupitia mfumo huu, mteja analipa kwa utaratibu rasmi, ambapo kodi za Serikali na ada ya wakala zinashughulikiwa kwa uwazi. Hii inapunguza migogoro ya malipo na kuongeza uaminifu katika mnyororo mzima wa biashara.
Kwa upande wa faida kwa mawakala wa Forodha ni kwamba mfumo huo unaleta mabadiliko makubwa kwa mawakala wa forodha. Kwanza, unahakikisha wakala analipwa kwa wakati, hivyo kupunguza madeni na migogoro iliyokuwa ikiathiri biashara zao.
Pili, unajenga mazingira ya ushindani wa haki. Badala ya kushindana kwa kushusha bei kupita kiasi, mawakala watashindana kwa ubora wa huduma, utaalamu na matumizi ya teknolojia.
Tatu, historia ya mapato inayopatikana kupitia mfumo inaweza kuongeza uwezo wa mawakala kupata mikopo, kuvutia wawekezaji na kupanua biashara zao.
Nne, taaluma ya uwakala wa forodha inapata hadhi zaidi kwa kuwa huduma zake zinasimamiwa kupitia mfumo rasmi unaotambulika.
Kwa upande wa faida kwa Waagizaji wa Mizigo watanufaika kwa kupata mfumo wenye uwazi na unaotabirika na kuongeza watakuwa na uelewa wa gharama wanazopaswa kulipa kabla ya huduma kukamilika, jambo litakalowasaidia kupanga bajeti na kupunguza migogoro.
“Aidha, kwa kuwa malipo ya wakala yanahakikishwa kupitia mfumo, huduma za utoaji wa mizigo zitafanyika kwa ufanisi zaidi na kwa muda mfupi.Hali hii itapunguza gharama za ucheleweshaji wa mizigo bandarini na kuongeza ushindani wa wafanyabiashara wa Tanzania katika soko la kikanda na kimataifa.
TAFFA imesema kwa Serikali, T-CAMS ni nyenzo muhimu ya kuongeza mapato na kuboresha usimamizi wa sekta. Mfumo unarahisisha ufuatiliaji wa miamala, unapunguza mianya ya ukwepaji kodi na unatoa takwimu sahihi kwa ajili ya kupanga sera na kuboresha huduma.
Aidha, uwazi wa miamala utaongeza uaminifu wa wawekezaji na taasisi za fedha katika mazingira ya biashara nchini.
Pia kuimarishwa ushindani wa Bandari za Tanzania Bandari za Tanzania zinashindana na bandari nyingine katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini. Mbali na miundombinu bora, ushindani huo unategemea pia kasi ya utoaji wa huduma na urahisi wa kufanya biashara.
“T-CAMS ni zaidi ya mfumo wa malipo. Ni mageuzi yanayolenga kujenga sekta ya uwakala wa forodha yenye uwazi, ushindani wa haki na ufanisi mkubwa.Kwa mawakala wa forodha, mfumo huu ni kinga ya malipo na daraja la kukuza biashara zao.
“Kwa waagizaji wa mizigo, ni njia ya kupata huduma bora na za uhakika. Kwa Serikali, ni nyenzo ya kuongeza mapato, kuimarisha usimamizi na kukuza biashara,”imesema taarifa ya TAFFA.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...