*KAWASIHI KUACHANA NA MAGENDO YA VITENGE NA KUPITA NJIA ILIYO RASMI

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kupitia idara Forodhaimee delea na zoezi la kutoa elimu kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa wadau wa forodha mkoani Songwe, ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uelewa kuhusu mabadiliko yaliyoanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2026/2027.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Meneja msaidizi Forodha mkoa wa Songwe, Afisa Forodha Mfawidhi wa Kituo cha Tunduma, Zahoro Makame, amesema mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha wadau kuelewa mabadiliko ya sheria mpya za kodi zilizoanza kutekelezwa mwezi Julai mwaka huu.

Makame amesema elimu hiyo ni muhimu kwa wadau wa forodha, wakiwemo mawakala wa forodha, wasafirishaji, wafanyabiashara na watumishi wa forodha, kwa kuwa mabadiliko hayo yanaathiri moja kwa moja namna taratibu za uingizaji na upelekaji wa bidhaa nje ya nchi zinavyotekelezwa.

Akifafanua kuhusu mabadiliko hayo,mwezeshaji ambaye ni Afisa Forodha Mfawidhi wa Mkoa wa Dodoma, Hassan Minga, amesema mabadiliko ya kibajeti yaliyofanywa kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2026 yamesababisha marekebisho katika sheria mbalimbali zinazohusiana na kodi na maeneo mengine ya biashara.

Minga amesema kwa upande wa forodha, kuna sheria kumi pamoja na kanuni moja zilizokumnwa na mabadiliko hayo. mapitio ya sheria moja ambazo zimeguswa na mabadiliko hayo, hatua inayolenga kukuza uchumi.
Kwa upande wake, Afisa Forodha Mkuu kutoka Kitengo cha Uwezeshaji Biashara Dar es Salaam, Alan Maduhu, amesema miongoni mwa mabadiliko hayo kuna hatua zinazowapa wafanyabiashara unafuu wa kodi, ikiwemo kupunguzwa kwa kiwango cha kodi kinachotozwa kwenye bidhaa ya vitenge vivyoingizwa nchini.
Maduhu amesema kodi ya vitenge ambayo awali ilikuwa ikitozwa kwa kiwango cha asilimia 50, sasa imeshushwa hadi asilimia 35 kuanzia mwaka huu wa fedha, akieleza kuwa wafanyabiashara wanapaswa kufahamu mabadiliko hayo ili waweze kufanya biashara kwa kuzingatia sheria.

Akihitimisha mafunzo hayo, Maduhu amewataka mawakala wa Forodha na Wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa toka nje ya nchi hasa kupitia mpaka wa Tunduma kutumia utaratibu wa kutengeneza Kadhia kabla ya mzigo kufika (PAD) ili kuwezesha uondoshwaji wa mizigo kwa haraka na kuepusha msongamano wa magari ya mizigo.

Kwa upande wao Mawakala wa Forodha walioshiriki mafunzo hayo, wameishukuru serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania kuwasogezea elimu hiyo muhimu na kuahidi kuwa mabalozi wa mabadiliko hayo ili kukuza biashara kupitia mpaka wa Tunduma ambao ni lango la SADC.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...