SAME.
ZAIDI ya watu 20 wanahojiwa na Jeshi la Polisi wilayani Same mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za kudaiwa kuendesha shughuli za uchimbaji haramu wa madini katika vyanzo vya maji ndani ya mita 60 kinyume cha sheria na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
Akizungumza kuhusu hatua zinazochukuliwa jana ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni, alisema Kamati ya Usalama ya wilaya ilipata taarifa za siri kuhusu uchimbaji huo katika maeneo mbalimbali na kufika kujiridhisha, ambapo ilibaini kuwepo kwa shughuli hizo.
Alisema baada ya kubaini hali hiyo, Kamati iliunda timu ya kwanza ya wataalamu kutoka RUWASA, Bodi ya Maji Bonde la Pangani, Maafisa Mazingira na Maafisa Madini, iliyofanya uchunguzi katika maeneo yote na kubaini uchimbaji haramu katika kata saba pamoja na uharibifu mkubwa wa mazingira.
Kasilda alisema kuwa, iliundwa timu ya pili kutoka ndani ya Kamati ya Usalama kwa ajili ya kuwabaini wahusika waliotajwa katika taarifa za siri zilizotolewa na wananchi na baadhi ya madiwani wenye nia njema na wazalendo.
“Hadi sasa zaidi ya watu 20 wanaotuhumiwa kuhusika na uchimbaji huo pamoja na kupeleka mitambo wamehojiwa na Jeshi la Polisi, na wengine wanaendelea kuhojiwa kwa awamu ili kupata ushahidi na watakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kisheria, na viongozi wa Serikali watakaobainika pia watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma,” alisema Kasilda.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema hali kama hiyo iliwahi kutokea mwaka 2023, ambapo Kamati ya Usalama ilitembelea maeneo hayo na kufanikiwa kuwakamata zaidi ya watu watano waliokuwa wakijihusisha na uchimbaji haramu pamoja na mitambo yao, hali iliyofanya shughuli hizo kusitishwa kwa muda hata hivyo, alisema uchimbaji huo umeibuka tena mwaka huu na hatua za kuwadhibiti zinaendelea.
Pia, wachimbaji hao wamebainika kufanya shughuli za uchimbaji bila kuwa na vibali wala leseni kutoka kwenye mamlaka husika huku, Kasilda akiwaonya watu wanaopanga kurejea katika maeneo hayo na kuendelea na uchimbaji haramu, akisisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watakaokiuka taratibu.
Kasilda alizitaka taasisi za Serikali zinazohusika na uhifadhi wa mazingira na ulinzi wa vyanzo vya maji kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na kuchukua hatua za kisheria.
Pia amewapongeza wananchi na baadhi ya madiwani waliotoa taarifa za siri na kusisitiza kuwa Serikali itawalinda.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, SACP Saimon Maigwa alisema kuwa, Jeshi hilo limeshafungua jalada na kwa sasa linaendelea na uchunguzi ili kubaini ukweli wa jambo hilo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...