Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho (Mb), amefanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Shirika la Tanzania Automotive Technology Centre (TATC), maarufu kama NYUMBU, lililopo Kibaha, Mkoa wa Pwani, kwa lengo la kujionea utendaji na utekelezaji wa majukumu yake.
Katika ziara hiyo, alitembelea maeneo mbalimbali ya shirika hilo linalomilikiwa na JWTZ na kuzungumza na uongozi wake ukiongozwa na Mwenyekiti, Luteni Jenerali na Balozi mstaafu Paul Meela. Dkt. Nyansaho aliupongeza uongozi wa NYUMBU kwa kazi zinazofanyika na kusisitiza shirika hilo liendelee kuongeza mchango wake katika uchumi, maendeleo ya teknolojia na ustawi wa Taifa.
TATC (NYUMBU) ni shirika la umma chini ya Wizara ya Ulinzi na JKT linalojihusisha na utengenezaji, ukarabati na ubunifu wa teknolojia katika eneo la vyombo vya moto, vipuri na vifaa vya uhandisi.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...