Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndg. Abdi Mahmoud Abdi, amewasili katika Tawi la CCM Kidoti, Jimbo la Nungwi, na kufanya mazungumzo na viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho.

Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa ukaguzi wa uhai wa CCM unaofanyika kuanzia ngazi ya matawi hadi majimbo, kwa lengo la kuimarisha chama na kuhakikisha shughuli zake zinatekelezwa kwa ufanisi.

Akizungumza na wanaCCM hao, Ndg. Abdi amewataka wanachama kuendelea kulipa ada zao za uanachama kwa wakati, akisisitiza kuwa ulipaji wa ada ni miongoni mwa wajibu muhimu unaochangia kukifanya chama kuwa imara na hai.

Amesema ushiriki wa wanachama katika kutekeleza wajibu wao utasaidia kuongeza uwezo wa CCM kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho na kusimamia utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa viongozi na wanachama kuendelea kushirikiana, kusikilizana na kudumisha mshikamano ili kuongeza ufanisi wa shughuli za chama katika ngazi zote.

Kwa upande wake, Katibu wa Kamati Maalum wa Idara ya Oganaizesheni CCM Zanzibar, Ndg. Omar Ibrahim Kilupi, amewataka wanaCCM kuendelea kujiandikisha na kupata Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi, hatua itakayowawezesha kujiandaa kutimiza haki yao ya msingi ya kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2030.

Ndg. Abdi anaendelea na ziara yake katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya kukagua uhai wa CCM, huku akikutana na viongozi na wanachama kwa lengo la kusikiliza changamoto zao, kuimarisha mshikamano na kuongeza ufanisi wa shughuli za chama.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...