SAME
MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki, Anna Kilango Malecela, amesema kuwa ili jimbo hilo liweze kukuza uchumi wake, ni muhimu Serikali kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kisiwani–Mkomazi kwa kiwango cha lami.
Kilango aliyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Soko la Kariakoo, Kata ya Ndungu, wilayani Same, wakati akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Aggrey Mwanri.
Alisema kuwa amekuwa akiwasilisha ombi la ujenzi wa barabara hiyo kwa Serikali tangu mwaka 2000, alipokuwa Mbunge wa Kuteuliwa na Rais, na kwamba juhudi hizo zimezaa matunda baada ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuipitisha barabara hiyo kujengwa kwa kiwango cha lami.
“Kwa sasa mkandarasi mmoja amepewa fedha kidogo kidogo, lakini sasa amepewa Sh bilioni 1.5 na ameanza kwa nguvu kuijenga barabara hii kwa kiwango cha lami,” alisema Kilango.
Aliongeza kuwa ataendelea kuisimamia kwa karibu kutokana na kuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Miundombinu inayohusika na masuala ya ujenzi wa barabara.
“Naomba niwahakikishie kuwa barabara yenu itajengwa. Imeipitishwa na Serikali, hivyo tumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu barabara hii ndiyo itakayosaidia kuleta uchumi wa Jimbo la Same Mashariki,” alisema.
Aidha, Kilango alisema wananchi wa Same Mashariki wanaendelea kukiunga mkono CCM kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika jimbo hilo.
Alisema jimbo hilo limepokea jumla ya Sh bilioni 54.349 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kwa mujibu wa Kilango, tangu alipoanza kipindi chake cha pili cha ubunge Januari mwaka huu, jimbo hilo limepokea Sh bilioni 44.3 kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa la Yongoma.
Alisema ujenzi wa bwawa hilo utawanufaisha wananchi wa Maore, Ndungu na Kihurio kwa kuwa utawawezesha kulima mpunga, kuongeza kipato na kukuza uchumi wao.
“Wananchi wa Jimbo la Same Mashariki ni wakulima wazuri, hivyo ujenzi wa bwawa hili utawanufaisha wananchi wa Maore, Ndungu na Kihurio kwa kuwa wataweza kulima mpunga na kujipatia kipato,” alisema.
Alitaja baadhi ya miradi mingine iliyopatiwa fedha na Serikali ya Awamu ya Sita kuwa ni ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Amali-Malecela, Kata ya Kihurio, uliogharimu Sh milioni 584.280; ujenzi wa Kituo cha Afya Vuje, Sh milioni 250; na upanuzi wa Kituo cha Afya Vunta, Sh milioni 629.996.
Miradi mingine ni upanuzi wa miundombinu ya Kidato cha Tano katika Shule ya Sekondari Misufini-Goma, Sh milioni 389.4; uboreshaji wa Skimu ya Umwagiliaji Kata ya Ndungu, Sh bilioni 6.988; pamoja na ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari ya Mkapa, Kata ya Ndungu, Sh milioni 584.280.
Miradi hiyo pia inahusisha fedha za kuchochea jitihada za maendeleo ya wananchi kiasi cha Sh milioni 53.490; ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Kidaru, Sh milioni 161.3; ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Msoroha, Sh milioni 187.3; ujenzi wa nyumba ya walimu yenye vyumba viwili katika Shule ya Msingi Mgandu, Sh milioni 100.841; na ujenzi wa madarasa manne pamoja na matundu tisa ya vyoo katika Shule ya Msingi Kigulunde, Sh milioni 120.378.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...