Na Hassan Kimweri, WAF – New York
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe, amesema Tanzania inaendelea kuchukua hatua madhubuti za kukabiliana na changamoto za magonjwa ikowemo saratani ya mlango wa kizazi kwa kuimarisha chanjo, uchunguzi wa mapema, utambuzi na matibabu ya ugonjwa huo kwa wakati.
Dkt. Magembe ameyasema hayo Septemba 23, 2026 pembezoni mwa Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) jijini New York, Marekani katika mkutano wa ngazi ya juu wa wadau ulioandaliwa na 'Business Council for International Understanding' (BCIU) ambao umelenga kuharakisha juhudi za kutokomeza saratani ya mlango wa kizazi.
"Tanzania imepiga hatua katika lengo la kwanza la mkakati wa kimataifa wa 90-70-90, ambapo zaidi ya asilimia 95 ya wasichana wamefikiwa na chanjo dhidi ya Virusi vya Human Papilloma (HPV), lakini pia kuna umuhimu wa kuongeza kasi katika uchunguzi na matibabu," amesema Dkt. Magembe
Aidha, Dkt. Magembe amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inaendelea kuongeza uwekezaji na kupanua huduma za uchunguzi, hususan maeneo ya vijijini, ikiwemo kutumia mfumo wa wanawake kujichukulia sampuli za HPV DNA ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hizo.
Katika hatua nyingine, Dkt. Magembe amesema Serikali imesambaza vifaa 359 vya 'thermocoagulation' na mashine 33 za LEEP, huku wataalamu 4,032 wa afya wakipatiwa mafunzo ya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi.
Pia, amesema, Serikali ya Tanzania inaendelea kujaribu matumizi ya teknolojia ya akili mnemba (AI), ikiwemo mfumo wa SEVIA, katika kuboresha huduma za uchunguzi.
Mwisho, Dkt. Magembe amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa Serikali, sekta binafsi, wadau wa maendeleo na jamii katika kuondoa unyanyapaa na kuongeza uhitaji wa huduma, ambapo Tanzania inalenga kuhakikisha kila msichana anapata chanjo, kila mwanamke anapata uchunguzi bora na kila anayehitaji matibabu anapata huduma kwa wakati na kwa gharama nafuu kupitia mpango wa Bima ya Afya kwa wote.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...