Kampeni ya Bonge la Wakala ya CRDB imechochea ushindani mkubwa miongoni mwa mawakala wa benki hiyo huku waliofanya vizuri zaidi katika kuongeza idadi ya miamala wakizawadiwa pikipiki 33 na mashine za POS 55  katika kipindi cha miezi mitano tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo.

Akizungumza mjini Morogoro wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi hizo, Mkurugenzi wa Matawi wa CRDB Bank Tanzania, Bonaventura Paul Kiungo, amesema kampeni hiyo imechangia kuongeza mapato ya benki kwa asilimia 8, huku matumizi ya maeneo ya mawakala katika utoaji wa huduma kwa jamii yakifikia asilimia 90.

Amesema hali hiyo imesaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha na kutimiza mahitaji ya wateja katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika zoezi hilo, jumla ya pikipiki 33 na mashine za POS 55 zilikabidhiwa kwa mawakala walioibuka washindi baada ya kufanya idadi kubwa ya miamala katika kipindi cha miezi mitano tangu kuanzishwa kwa kampeni ya Bonge la Wakala.

Kiungo amesema utoaji wa zawadi hizo ni sehemu ya malengo ya CRDB ya kuhamasisha mawakala kuongeza juhudi katika utoaji wa huduma na kupanua wigo wa huduma za benki kwa wananchi.

Ameongeza kuwa kampeni hiyo itaendelea kuwa endelevu, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo kukuza mtandao wa mawakala na kuhakikisha wateja wanapata huduma kwa urahisi zaidi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawakala wa CRDB, Abbas Abrahiman, amesema kampeni hiyo imeongeza chachu na ushindani miongoni mwa mawakala, hali ambayo imekuwa na mchango katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja.

Naye Ester Raphael, mmoja wa mawakala walionufaika na zawadi hizo, amesema pikipiki waliyopewa itasaidia kuongeza ufanisi na ubora wa huduma kwa wateja, hasa katika kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.

Kampeni ya Bonge la Wakala inalenga kuhamasisha mawakala kuongeza idadi ya miamala, kuboresha huduma na kuchochea matumizi ya huduma za kifedha kupitia mtandao wa mawakala wa CRDB nchini.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...