WASUSI mbalimbali nchini wameipongeza Kampuni ya Darling Hair kwa kuwawezesha kiuchumi na kuwakwamua kutoka kwenye umaskini kupitia programu yake maalumu inayofahamika kama Loyalty.

Pongezi hizo zilitolewa katika hafla maalumu iliyofanyika Sinza, Jijini Dar es Salaam na kuwakusanya mamia ya wasusi katika hafla maalumu ya kupongezana na kutoa zawadi mbalimbali iliyoandaliwa na Darling Hair na kuhudhuriwa na uongozi wa juu kabisa wa kampuni hiyo.

“Kupitia program hii Darling Hair imetusaidia sana sisi kama wasusi na wenye masaluni kwani sasa hivi hatununui vifaa hasa viti. Tunakusanya lebo za bidhaa mbalimbali za Darling Hair na kujikusanyia pointi mbalimbali zinazotuwezesha kushinda zawadi mbalimbali,” alisema Veronica Millinga, mmoja wa wasusi aliyehudhuria hafla hiyo.

Alitoa wito kwa wasusi ambao hawajajiunga na program hiyo kuchangamkia fursa hiyo kwani faida zake ni nyingi ikiwemo baadhi ya wasusi wadogo kufungua saluni zao wenyewe.

Naye Ramadhani Kataya ambaye ni msusi na mmiliki wa saluni, alisema kupitia programu hii Darling Hair imejiweka karibu sana na wateja wake na inafuatilia hatua kwa hatua ili kuhakikisha wanapata huduma bora.

“Hawa Darling ni wabunifu sana hata mteja akija na hitaji fulani kwa haraka tu unafahamu kuwa Darling Hair wana suluhisho na ukiwapigia wanakuhudumia haraka,” alisema.

Rukia Adam, ambaye pia ni msusi, alisema program hiyo ya Loyalty imewasaidia wasusi wengi wadogo na kuwafanya wajiamini zaidi kwa kuwapa mitaji ya vifaa mbalimbali vya saluni.

“Kwa kweli wametuwezesha sana na tunaomba programu hii iwe ya kudumu ili wengi zaidi wafadike na pia itunyanyue kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine,” alisema.

Meneja Saluni wa Darling Hair, Joyce Mwijage, alisema, awamu ya kwanza ya programu hiyo ilipata mafanikio makubwa ambapo idadi ya wasusi iliongezeka kutoka 5000 hadi 15,000.

Alisema hafla hii iliyowakusanya wasusi kutoka Tegeta, Wazo, Makonde, Boko, Bunju, Tanki Bovu, Mivumoni, Kunduchi na Kawe ni ya pili tangu kampuni hiyo izindue awamu ya pili ya program hiyo iliyoanza 2024. “Baada ya Dar es Salaam tutaenda mikoa mbalimbali ili tuwafikie wasusi nchi nzima,” alisema.

Alisema washiriki walikusanya lebo za bidhaa za Darling Hair na kujizolea pointi kadhaa ambazo ziliwawezesha kujipatia zawadi mbalimbali.

“Lengo la program hii ya Loyalty ni kuwazawadia wasusi wadodo wadogo ili waweze kujiendeleza na hatimaye kufungua saluni zao wenyewe kutokana na vifaa vya saluni wanavyojishindia kwa kukusanya lebo za bidhaa zetu na kujizolea pointi kwa kila lebo.”Alisema.

Aliongeza kuwa baada ya Dar es Salaam.watahamia katika mikoa mingine ambapo amewataka wasusi hao kujipanga kwa kampeni hiyo ambayo kwa mujibu wa meneja huyo, ni ya kudumu.

Kulikuwa na zawadi, michezo mbalimbali, mziki uliopambwa na wasanii mbalimbali akiwemo msanii maarufu, Click Master ambaye hakuwaangusha mashabiki wake kwa kuimba nao nyimbo kama Watajua na Sherehe.
Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...