Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, leo Septemba 30, 2026, ameendelea kuongoza kikao kazi cha kuwajengea uwezo Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi, mikoa, vikosi na vyuo vya polisi.
Kikao hicho kinafanyika katika ukumbi wa Shule ya Polisi Tanzania, Moshi, na leo kimeingia siku ya tatu tangu kuanza kwa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo ya siku tatu yanalenga kuwajengea uwezo Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi, hususan katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya usalama na kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ushirikiano huo ni muhimu katika kubaini na kuzuia uhalifu, pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kabla hazijakua na kuwa matukio ya uhalifu.
Aidha, kikao hicho kinalenga kuwawezesha Maafisa Habari kuimarisha mahusiano na vyombo vya habari, huku wakizingatia mabadiliko ya mazingira ya mawasiliano yanayotokana na maendeleo ya teknolojia.
Mafunzo hayo pia yanatarajiwa kuwaongezea uwezo Maafisa Habari katika kutumia mbinu na njia mbalimbali za mawasiliano zinazokidhi mahitaji ya sasa, ili kuhakikisha taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu masuala ya usalama zinawafikia wananchi.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...