Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema matumizi ya takwimu rasmi yana nafasi muhimu katika kutambua fursa za uwekezaji, kufanya maamuzi sahihi na kupanga shughuli mbalimbali katika sekta ya madini nchini.
Akizungumza leo Septemba 30, 2026, mkoani Geita katika Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini, Meneja wa NBS Mkoa wa Geita, Khalid Mohamed Msabaha, amesema takwimu rasmi zinaisaidia serikali, wafanyabiashara na wadau wa maendeleo kupanga shughuli zao kwa kuzingatia taarifa sahihi.
Amesema sekta ya madini imeendelea kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa, ambapo mwaka 2025 mchango wa sekta hiyo katika Pato la Taifa ulifikia asilimia 10.3, kutoka asilimia 9 kwa mwaka uliopita.
Kwa mujibu wa Msabaha, kuendelea kwa shughuli za madini mkoani Geita kumechochea fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwemo biashara, ajira na shughuli zinazohusiana na mnyororo wa thamani wa sekta ya madini.
Amesema NBS imeshiriki maonesho hayo ili kutoa elimu na kuwawezesha wananchi pamoja na wadau mbalimbali kupata takwimu rasmi zinazohusu idadi ya watu, uchumi, afya, kilimo na maeneo mengine.
Amesema hadi mwaka 2026, Mkoa wa Geita unakadiriwa kuwa na takribani watu milioni 3.4, hali inayochangiwa kwa kiasi kikubwa na fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na shughuli za madini, ikiwemo biashara, ajira na shughuli za uchimbaji wa madini.
Ameongeza kuwa wafanyabiashara na wawekezaji wanaotaka kufanya shughuli mbalimbali mkoani Geita na maeneo mengine nchini wanaweza kutumia takwimu hizo katika kufanya maamuzi na kupanga mipango ya uwekezaji.
NBS pia imewahamasisha wananchi na wadau mbalimbali kupata takwimu rasmi kupitia tovuti yake na kurasa zake za mitandao ya kijamii, hatua inayolenga kuongeza matumizi ya takwimu katika shughuli za maendeleo.
NBS imewataka wananchi na wadau mbalimbali, kutembelea banda lake katika Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Sekta ya Madini mkoani Geita, ambapo watapata fursa ya kupata takwimu rasmi na maelezo mbalimbali yanayoweza kuwasaidia katika kupanga, kufanya maamuzi na kutambua fursa za kiuchumi na uwekezaji, kulingana na idadi ya watu katika eneo husika.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...