Katibu wa NEC – Uchumi na Fedha wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Jamal Kassim Ali, leo tarehe 6 Septemba 2026 amezindua rasmi mradi wa vibanda vya biashara kwa wajasiriamali wadogo unaomilikiwa na CCM Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mradi huo, Ndugu Jamal ameipongeza CCM Mkoa wa Kagera kwa kutumia rasilimali za Chama kuanzisha mradi wenye tija, unaolenga kuchochea shughuli za kiuchumi, kuwawezesha wajasiriamali wadogo na kuongeza uwezo wa Chama katika kujitegemea.

Amesema wajasiriamali wadogo wa leo ndio msingi wa wawekezaji wakubwa wa kesho, hivyo amewataka viongozi, hususan madiwani, kutambua na kutumia fursa za kiuchumi zilizopo katika kata zao ili kuwawezesha vijana kujiajiri na kujenga uchumi wa maeneo yao.

Aidha, Ndugu Jamal amewataka wanachama wa CCM kuishi kwa vitendo Imani na misingi ya Chama, akisisitiza umuhimu wa nidhamu, usawa na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu ya Chama.

Amesema hakuna mwanachama aliye juu ya Chama, na kwamba kila mwanachama anapaswa kuheshimu Katiba, kanuni na taratibu za CCM bila kujali nafasi au cheo alichonacho.

“Hakuna mtu aliye juu ya CCM; wanachama wote ni sawa mbele ya Katiba, kanuni na taratibu za Chama.”






Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...