-Mpango wa dampo la Pugu kushirikisha sekta binafsi waiva… madiwani watoa msimamo
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limekutana katika kikao maalum kilichokuwa na lengo la kutekeleza maagizo ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuhusu kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya uchafu katika Jiji hilo.
Katika kutekeleza maagizo hayo pamoja na mambo mengine kikao hicho kilichoongozwa na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Nurdin Bilal maarufu Shetta pamoja na Katibu wa kikao hicho ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji hilo Elihuruma Mabelya wamekubaliana kushirikisha sekta binafsi kupitia mpango wa PPP kuendesha dampo la Pugu kinyamwezi ambalo kwa sasa limezidiwa.
Katika kikao hicho maalum kilichofanyika leo Septemba 4,2026 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya amewasilisha mpango wa kushirikiaha sekta binafsi kusimamia dampo la Pugu Kinyamwezi ambalo ndilo linatumika kutupwa taka zote zinazozalishwa katika Jiji hilo.
“Kumekuwa na mpango mkakati wa Jiji la Dar es salaam unaotaka asilimia 80 ya taka zipelekwe dampo la Pugu na ukweli mpango huo umefeli.Kutokana na ongezeko la watu katika Jiji la Dar es Salaam umefika wakati wa kushirikisha sekta binafsi kupitia PPP ili kupata suluhu ya kudumu.”
Akifafanua zaidi katika kikao hicho Mabelya amesema maagizo yaliyotolewa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan yanapaswa kutekelezwa kwa haraka na jambo muhimu zaidi kuwa na suluhu ya kudumu.
“Tumepokea maagizo ya Rais Samia lakini pia Spika wa Bunge ameonesha kutoridhishwa n hali ya usafi katika Jiji la Dar es Salaam.Tumewasikia viongozi wetu na tumechukua hatua mbalimbali na leo tumekutana katika kikao maalum kujadili maagizo tuliyopewa.”
Kuhusu taka zinazozalishwa katika Jiji la Dar es Salaam amesema kwa siku zinazalishwa kiasi cha taka tani 1320 kwa siku na zinazopelekwa dampo la Pugu ni tani 792 pekee wakati taka zinaozalishwa katika halmashauri zote ni kati ya tani 2500 hadi 3000 kwa siku.”Taka nyingi bado zipo mtaani na zinaathiri wanannchi kiafya na mazingira.”
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amepongeza kufanyika kikao hicho kutekeleza maagizo ya Rais na kusisitiza Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam linamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kusema ukweli kuhusu hali ya usafi katika Jiji hilo.
“Ni heshima kubwa kwa Kiongozi akishatoa maagizo kuona maagizo yanatekelezwa.Niwapongeze Baraza l madiwani kwa kikao hichi kilichokutana kutekeleza maagizo tuliyopewa.”
Pamoja na hayo amesema changamoto ya dampo la Pugu halmashauri imekuwa inatumia nguvu nyingi katika dampo hilo na mashine za kushusha taka zimekufa.
“Mtu anayekwambia ukweli anakupenda,hali ni mbaya.Heka 400 kabla ya kuingia dampo taka kila mahali na kwa miaka minne kumekuwa na siasa nyingi kuhusu dampo hilo..Nawapongeza kwa kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan.
“Spika amesema bungeni wapi ambapo wakandarasi wanakwamisha.Tunajua mpango huu mzuri wa kushirikisha sekta binafsi katika dampo letu kuna watu watanuna kwa maslahi yao binafsi. Hivyo kazi ambayo imebakia ni watalaam kukaa na kuona jinsi mikataba itakavyokuwa kwani kuingia PPP kuna mikataba ya kisheria .
“Rais amezungumza miaka yote tunakwenda tunarudi nyuma jambo halifiki mwisho kama tumekanyaga mdudu.Sasa twendeni tukatekeleze mpango huu wa dampo na dira ya 2050 inaeleza umuhimu wa kushirikisha sekta binafsi katika kutekeleza mipango ya Serikali.”

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...