Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, amemkabidhi kompyuta Afisa Mteule Daraja la Pili Nassoro Kapiga, Kaimu Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Ubungo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Luguruni, ambapo Mhe. Kairuki amekabidhi kompyuta hiyo kwa lengo la kusaidia kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Afisa Mteule Daraja la Pili Nassoro Kapiga.
Kompyuta hiyo inatarajiwa kuwa nyenzo muhimu katika shughuli za kiutendaji, ikiwemo utunzaji wa taarifa, maandalizi ya nyaraka na matumizi ya teknolojia katika kutekeleza majukumu yake kama Kaimu Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Ubungo.
Makabidhiano hayo yanaelezwa kuwa sehemu ya kuunga mkono matumizi ya teknolojia katika kuboresha utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu.Kwa upande wake, Afisa Mteule Daraja la Pili Nassoro Kapiga amemshukuru Mheshimiwa Kairuki kwa msaada Huo.

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...