TUMBATU, ZANZIBAR — Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, amekagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tumbatu, akieleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutarahisisha upatikanaji wa huduma za afya, ikiwemo huduma za kibingwa, kwa wananchi wa Kisiwa cha Tumbatu.

Akitoa taarifa ya kitaalamu wakati wa ziara hiyo, msimamizi wa mradi amesema hospitali hiyo itatoa huduma mbalimbali za afya, zikiwemo huduma za afya ya jamii na huduma za kibingwa, hatua itakayosaidia kupunguza changamoto ya wananchi kusafiri nje ya kisiwa kufuata huduma hizo.

Wananchi wa Tumbatu wamempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kwa kuendelea kutekeleza ahadi za Serikali kwa vitendo, hususan katika kuimarisha huduma za kijamii na afya.

Kwa upande wake, Ndugu Abdi amempongeza Dkt. Mwinyi kwa hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika kuimarisha huduma za afya katika Kisiwa cha Tumbatu, huku akisisitiza umuhimu wa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika na huduma zinazotarajiwa.

Aidha, amewataka madaktari na watumishi wa afya kuhakikisha wanatoa huduma bora, zenye weledi na zinazozingatia mahitaji ya wananchi, akisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya na kuimarisha ustawi wao.

📆 16 Septemba, 2026
📍 Tumbatu, Zanzibar.










 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...