Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umeendelea kuvuna matunda ya uwekezaji katika utalii wa misitu, huku idadi ya watalii wanaotembelea vivutio vinavyosimamiwa na taasisi hiyo ikifikia 377,116 mwaka 2025, ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka watalii 46,533 mwaka 2020.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Utalii TFS, PCO Someni Mteleka, ongezeko hilo linaenda sambamba na kuimarika kwa mchango wa utalii katika mapato ya taasisi, ambapo mwaka 2020 TFS ilirekodi watalii mapato ya zaidi ya Sh 159 milioni kutokana na utalii wa ikolojia na kuongezeka hadi Sh 3.5 bilioni mwaka 2025/2026

Akizungumza jana Septemba 15, 2026 jijini Dodoma wakati wa mafunzo ya utangulizi kwa watumishi wapya wa TFS, Mteleka alisema taasisi hiyo inaendelea kuendeleza bidhaa mbalimbali za utalii zinazotokana na misitu, mashamba ya miti, mikoko na maeneo ya kihistoria, hatua inayolenga kuongeza fursa za utalii na manufaa ya kiuchumi.

Alisema TFS kwa sasa inasimamia maeneo 35 ya utalii yanayotoa shughuli mbalimbali, zikiwemo matembezi ya misituni, kuangalia ndege na wanyama, kupanda na kutalii milimani, utalii wa nyuki, baiskeli, kuendesha mitumbwi na kayak, kambi, picnic, pamoja na kutembelea maeneo ya kihistoria na kitamaduni.

Mteleka alisema ukuaji wa utalii umechangiwa pia na kuongezeka kwa maeneo ya hifadhi za misitu ya kitaifa (NFRs), ambayo yameongezeka kutoka maeneo matano mwaka 2015 hadi kufikia 25 mwaka 2025, huku utalii wa ikolojia ukiwa miongoni mwa shughuli kuu za kiuchumi zinazoruhusiwa katika maeneo hayo kwa kuzingatia uhifadhi na athari ndogo kwa mazingira.

Alisema mbali na hifadhi za misitu, TFS inaendelea kutumia mashamba ya miti na misitu ya mikoko kuendeleza bidhaa mpya za utalii zisizohitaji uvunaji wa rasilimali, ikiwemo utalii wa michezo kama mbio za magari, marathoni na shughuli za kuendesha farasi, pamoja na shughuli za utalii katika maeneo ya mikoko.

Kwa mujibu wa Mteleka, TFS pia inasimamia vituo sita vya maeneo ya kale, vikiwemo Mji Mkongwe wa Bagamoyo, Magofu ya Kaole, Tongoni, Michoro ya Miamba ya Kondoa ambayo ni eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO, pamoja na maeneo yanayohusishwa na Dk. David Livingstone na Jengo la Afya.

Alisema TFS inaendelea kushirikiana na taasisi za Serikali, washirika wa maendeleo, mashirika yasiyo ya Serikali, jamii na sekta binafsi katika kuboresha miundombinu, huduma na upatikanaji wa vivutio, huku ikiendelea kutangaza bidhaa zake kupitia vyombo vya habari vya jadi na kidijitali ili kuongeza watalii na kuchangia lengo la taifa la kufikia watalii milioni nane kwa mwaka ifikapo 2030.





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...