Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Ndugu Rabia Abdalla Hamid, amewahimiza wananchi kutumia kikamilifu fursa mbalimbali zinazotengenezwa na kuwezeshwa na Serikali ili kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Rabia ametoa rai hiyo leo, Septemba 21, 2026, wakati akiendelea na ziara ya CCM katika Mkoa wa Iringa, yenye lengo la kusikiliza, kuzungumza na wananchi pamoja na kufuatilia na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa makundi mbalimbali ya kijamii.

Katika ziara hiyo, Rabia amepata fursa ya kusikiliza changamoto na mahitaji mbalimbali ya wananchi, huku akiwahimiza kuwa na utayari wa kutumia fursa zinazopatikana kupitia mipango na programu mbalimbali za Serikali.

Amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa CCM, imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wananchi kushiriki katika shughuli za kiuchumi na kijamii, hivyo ni muhimu kwa wananchi kuzitambua na kuzitumia fursa hizo kwa maendeleo yao binafsi, familia na jamii kwa ujumla.

Rabia amesisitiza kuwa juhudi za Serikali katika kuwawezesha wananchi zitakuwa na tija zaidi iwapo wananchi wenyewe watazitumia fursa hizo kwa kuongeza uzalishaji, kuanzisha na kuendeleza shughuli za kiuchumi pamoja na kutumia fursa za uwezeshaji zinazotolewa na Serikali.

Amesema CCM itaendelea kusimamia na kuhamasisha utekelezaji wa sera na mipango yenye lengo la kuboresha maisha ya wananchi na kuhakikisha fursa za maendeleo zinawafikia makundi mbalimbali katika jamii.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...