Na Janeth Raphael - MichuziTv
Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uganda, umefikia asilimia 92.7 ya utekelezaji huku Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ikiwa na umiliki wa asilimia 15 katika mradi huo.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga nchini Tanzania, ambapo hatua mbalimbali za ujenzi zinaendelea kuelekea kuanza kwa shughuli za uendeshaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Septemba 21, 2026, katika Ukumbi wa Idara ya Habari – MAELEZO, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mussa Makame, amesema utekelezaji wa EACOP umeendelea kutoa manufaa kwa Watanzania kupitia ajira, biashara, kandarasi na fursa za utoaji huduma.

Amesema katika kipindi cha ujenzi, jumla ya ajira 10,000 zimezalishwa, kati yake 7,500 sawa na asilimia 75 zikitolewa kwa Watanzania, huku zaidi ya kampuni 200 za Kitanzania zikipewa kandarasi za ugavi wa bidhaa na huduma zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Trilioni 1.325.
Kwa upande wa mapato, Makame amesema utekelezaji wa mradi huo umeiwezesha Serikali kukusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kupitia kodi, ada, ushuru na tozo mbalimbali.

Ameeleza kuwa mchango huo unatarajiwa kuongezeka zaidi baada ya mradi kuanza rasmi awamu ya uendeshaji, huku uwekezaji huo ukiendelea kuongeza ushiriki wa sekta binafsi ya ndani na kuchochea shughuli za kiuchumi katika maeneo yanayopitiwa na mradi.
Aidha, amesema EACOP imeendelea kutekeleza miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) katika maeneo ya elimu, afya na mazingira, ikiwemo mradi wa maji wenye thamani ya takribani Shilingi Bilioni 4.4 unaowanufaisha wananchi zaidi ya 26,000, ujenzi na uboreshaji wa huduma za afya katika Kata ya Chongoleani, pamoja na ugawaji wa miche ya minazi milioni mbili.

Mradi huo pia umejenga kituo cha kisasa cha michezo na kutoa mafunzo ya stadi za kazi kwa vijana 800 kwa lengo la kuwawezesha kujiajiri na kupata ajira katika sekta mbalimbali.
Akizungumzia ratiba ya hatua zinazofuata, Makame amesema TPDC inatarajia tone la kwanza la mafuta (First Drop) kuingia katika Pump Station No. 1 nchini Uganda mwezi Desemba 2026.

Baada ya hapo, mafuta ghafi yatasukumwa kupitia mfumo wa bomba kutoka Uganda hadi Tanzania kwa kipindi cha takribani miezi miwili na yanatarajiwa kufika Chongoleani, Tanga, mwezi Februari 2027, ambapo yatajazwa katika matenki manne yenye uwezo wa kuhifadhi kwa pamoja mapipa milioni mbili ya mafuta ghafi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...