Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka washiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Teknolojia na Akili Unde (Tech & AI International Expo 2026) kuyageuza majadiliano kuwa ushirikiano wenye matokeo kwa wananchi. Katika maonesho hayo, Yas Tanzania imesema itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya mawasiliano na kuchochea huduma za kidigitali visiwani Zanzibar.
Akifungua maonesho hayo leo katika hoteli ya Golden Tulip Zanzibar, Dkt. Mwinyi alisema teknolojia ina mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya, elimu na huduma za umma, pamoja na kufungua fursa za biashara na ajira.
“Maonesho haya yanatoa nafasi muhimu ya kubadilishana mawazo, kujenga ushirikiano, kuonesha ubunifu na kutafakari namna teknolojia inavyoweza kuchochea maendeleo yanayomfikia kila mmoja na kuijenga kesho yetu,” alisema.
Rais Mwinyi aliwataka wabunifu kutafuta suluhisho kwa changamoto zinazowakabili wananchi. Alisema manufaa ya teknolojia yanapaswa kuwafikia pia wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na wakazi wa maeneo ya pembezoni ambao hawajafikiwa na huduma.
Kwa upande wake, Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga, alisema vijana wanahitaji mazingira yatakayowawezesha kutumia ujuzi wa kidijitali kuanzisha biashara na kuhudumia wateja ndani na nje ya Zanzibar.
“Kijana wa Zanzibar anahitaji tu kuwa na wazo, kitendea kazi na huduma ya intaneti, kisha kujenga biashara inayohudumia wateja hapa nchini na hata nje ya mipaka yetu,” alisema.
Soraga alisema Serikali inaweka sera na kanuni zitakazosaidia kampuni changa za teknolojia kukuza biashara zao.
Naye, Ofisa Mkuu wa Biashara wa Yas Tanzania, Bw. Norman Kiondo, alisema kampuni hiyo itaendelea kuwekeza katika mtandao na kushirikiana na wadau kufikisha huduma za kidijitali kwa wananchi na biashara nyingi zaidi. Alisema kwa hapa Zanzibar, Yas inashirikiana na ZICTIA kupanua huduma za intaneti ya (faiba) kuchochea huduma ya intaneti majumbani, taasisi na biashara Zanzibar ambapo imewekeza zaidi ya Sh bilioni 300.
Kwa mujibu wa Kiondo, Yas vilevile, imewekeza zaidi ya Sh trilioni 1.2 katika mtandao wake nchini, na sasa ina zaidi ya minara 4,900 na zaidi ya kilomita 5,700 za miundombinu ya intaneti ya faiba.
Alisema mawasiliano bora Zanzibar yatawezesha biashara za utalii kuwahudumia wageni, wajasiriamali kuwafikia wateja na taasisi za umma kutoa huduma kwa urahisi zaidi.
“Tutaendelea kuwekeza na kuboresha miundombinu yetu ya mawasiliano ili kuwa na mtandao imara hapa Zanzibar. Pia tutaendelea kushirikiana na Serikali na taasisi mbalimbali kusaidia biashara kutumia teknolojia na kuchochea ubunifu,” alisema Kiondo

.jpg.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...