Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete, Septemba 14, 2026 amekabidhi magari mawili kwa Vikundi viwili vya wananchi ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia mikopo yenye masharti nafuu.

Magari hayo aina ya Basi la abiria na gari ndogo ya kubebea mizigo, yamekabidhiwa kwa vikundi hivyo ili kuwawezesha kufanya shughuli za kiuchumi zitakazosaidia kuongeza kipato na kuboresha maisha ya wanakikundi pamoja na familia zao.

Akizungumza wakati wa ziara yake ameonesha kufurahishwa na mmoja kati ya waliopatiwa magari hayo ni kutoka kikundi cha watu wenye ulemavu ambaye amepatiwa gari ndogo kwajili ya kubeba mizigo Mhe. Kikwete amesema mpango huo ni sehemu ya mwendelezo wa kuwawezesha wananchi kupata mitaji na vitendea kazi ambavyo vitawasaidia kujiajiri na kuongeza kipato.

Amesema wananchi wanaopatiwa fursa hiyo wanapaswa kutumia vizuri mikopo na vitendea kazi wanavyokabidhiwa ili viweze kuleta tija na kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.

Kwa mujibu wa Mhe. Kikwete, utaratibu huo unawawezesha wananchi kurejesha mikopo kidogo kidogo bila riba, jambo ambalo linawapa nafasi ya kuendesha shughuli zao bila kubanwa na gharama kubwa za marejesho.

Amesisitiza kuwa lengo la mpango huo si kutoa fedha pekee, bali ni kujenga uwezo wa wananchi kuwa na shughuli endelevu zitakazowawezesha kuongeza kipato na kukabiliana na changamoto za maisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...