Na Mwandishi Wetu - Arusha

Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Mhe. Jaji Mstaafu Hamisa Kalombola, ametoa wito kwa watumishi wa umma kutekeleza wajibu kwa uadilifu, uzalendo na uwajibikaji ikiwa ni pamoja na kuwahudumia wananchi kwa usawa sambamba na kuwa na maisha yenye taswira chanya katika jamii.

Mhe. Jaji (Mst) Kalombola, amesema hayo katika Kikao chake na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kilicholenga kuwakumbusha kuhusu haki, wajibu, maadili na misingi ya Utumishi wa Umma ambapo amesisitiza haki kuendana na wajibu

“utumishi wa umma hauishi ofisini, nendeni mkaiwakilishe vyema serikali kwenye utoaji wa huduma na maisha mnayoishi kwenye jamii’’ amehimiza Mhe. Jaji (Mst) Kalombola.

Kwa upande wake, Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Nolasco Kipanda, ameeleza Tume hiyo katika kuhakikisha sheria, kanuni, taratibu na misingi ya Utumishi wa Umma inazingatiwa kwenye mashirika na taasisi za umma inafanya ukaguzi ambapo hadi sasa umeyafikia mashirika na taasisi 90.

Mkurugenzi Mkuu TAWIRI, Dkt. Eblate Mjingo ameeleza taasisi hiyo inatambua mchango wa Tume katika kusimamia haki za watumishi na kwamba katika ari hiyo Taasisi imewasogeza karibu watumishi kwa kuhakikisha kupitia vikao vya maamuzi watumishi wanauwakilishi huru kupitia Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi katika tawi la taasisi ni mjumbe mbali na kuwakilishwa na wasimamizi wao.

Kikao hiko kimefanyika Makao Makuu ya TAWIRI Njiro - Arusha ambapo kimewakutanisha wajumbe waliongozana na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma,wajumbe wa Menejimenti ya TAWIRI na watumishi.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...